Show simple item record

dc.contributor.authorAnindo, Violet
dc.date.accessioned2022-04-28T07:54:25Z
dc.date.available2022-04-28T07:54:25Z
dc.date.issued2021
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/160343
dc.description.abstractHuu utafiti umechanganua mifanyiko ya kifonolojia ambayo hutokea kwenye maneno mkopo ya Kinyore kutoka Kiswahili. Tofauti baina ya Kiswahili na Kinyore ni kwamba Kiswahili kina silabi funge ambazo haziko katika Kinyore. Maneno yanapokopwa hupitia michakato mbalimbali ili kuafiki muundo wa maneno ya Kinyore. Kazi ambazo zimechapishwa katika fonolojia zina uchunguzi halisi wa kifonolojia ambao maneno mkopo hupitia lakini uchunguzi wenyewe ni mchache. Utafiti wetu ulilenga kujaza hili pengo. Mtazamo wa nadharia ya fonolojia leksika umeongoza huu uchunguzi. Kulingana na mtazamo huu uundaji wa maneno huanzia kwa maumbo ya ndani. Umbo la nje hutokana na umbo la ndani ambapo mzizi au shina huambishwa. Maneno mkopo hupitia mabadiliko mbalimbali ili yakubalike katika lugha pokezi na mabadiliko haya hutokea kwenye fonimu au silabi. Utafiti huu umethibitisha kuwepo kwa maneno mkopo ya Kiswahili katika Kinyore. Mifanyiko mbalimbali kama uchopekaji, udondoshaji na ugeuzaji maumbo imeonyesha jinsi maneno yanavyopitia mabadiliko ili yakubalike katika Kinyore. Baadhi ya irabu za maneno mkopo huimarika zinapoingizwa katika Kinyore. Maneno mkopo yaliyo na silabi ya muundo K yanapokopwa huo muundo hubadilika na kuwa KI kwa sababu Kinyore hakina muundo wa silabi wa K. Baadhi ya maneno yanapokopwa huambishwa irabu au silabi. Ukopaji umesaidia kukuza Kinyore kwani msamiati wa kufidia dhana geni umepatikana. Pia umesaidia kukuza irabu, konsonanti na silabi za Kiswahili. Utafiti huu umebainisha vigezo vya kifonolojia vilivyotumika na kuchanganua taratibu za kifonolojia na kimofolojia zilizofuatwa katika ukopaji. Uwasilishaji umefanywa kupitia njia ya maelezo, michoro na majedwali. Data ya matokeo ya uchunguzi wetu inaweza kusaidia wasomi wa isimu za lugha za kiafrika.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectFonolojia Ya Maneno Mkopoen_US
dc.titleFonolojia Ya Maneno Mkopo Ya Kinyore Kutoka Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States