Show simple item record

dc.contributor.authorYego, Mercy J
dc.date.accessioned2023-02-14T06:42:12Z
dc.date.available2023-02-14T06:42:12Z
dc.date.issued2022
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/162459
dc.description.abstractUtafiti huu unachanganua jinsi maneno yanavyokopwa na Kiarror kutoka lugha ya Kiswahili na kufanywa yakubalike kifonolojia na kimofolojia katika lugha ya Kiarror kwa kuzingatia muundo wa kisarufi wa lugha hiyo. Kiswahili na Kiarror huwa na mifumo tofauti ya kifonolojia na kimofolojia. Kwa mfano, utafiti huu ulibaini kuwepo kwa fonimu za Kiarror ambazo hazipo katika fonolojia ya Kiswahili, na vilevile kuwepo kwa fonimu za Kiswahili ambazo hazipo katika fonolojia ya Kiarror. Aidha, kuna tofauti baina ya miundo ya silabi pendelewa za Kiarror na silabi pendelewa za Kiswahili. Pia lugha hizi hutofautiana katika uambishaji wa maneno kiidadi. Kwa vile maneno yakopwayo sharti yazingatie masharti ya lugha kopaji ili yaweze kukubalika katika mfumo wa lugha kopaji, maneno yanapokopwa na Kiarror kutoka Kiswahili, hupitia michakato anuwai ya kifonolojia na ya kimofolojia ili yawe na miundo inayokubaliana na mfumo wa kimofofonolojia wa lahaja ya Kiarror. Licha ya utafiti huu kuchanganua michakato hiyo, ulilenga pia kubainisha sababu za michakato hiyo na athari zake katika maneno mkopo. Nadharia ambayo iliongoza utafiti huu ni nadharia ya fonolojia zalishi Asilia. Nadharia hii imetumika ili kueleza michakato ya kimofofonemiki inayohusika katika ukopaji na utohozi wa maneno mkopo ya lugha ya Kiarror kutoka lugha ya Kiswahili.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMofofonolojia Ya Maneno Mkopo Ya Kiarror Kutoka Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States