Show simple item record

dc.contributor.authorMutie, Edith K
dc.date.accessioned2013-05-02T06:41:32Z
dc.date.available2013-05-02T06:41:32Z
dc.date.issued1997
dc.identifier.citationT asnifu hii imetolew a ill kutosheleza baadhi y a mahit all y a shahada y a m.a. ka tika chuo kikuu cha Nairobien
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18189
dc.description.abstractKazi nyingi za tafsiri hudharniria kuiboresha tafsiri na athari zake katika Kiswahili; ikizingatia matatizo, makosa, dosari na athari zake juu ya fasihi kwa jumla. Uhakiki huu umejikita katika kazi moja ya kifasihi ambayo irnetafsiriwa katika Kiswahili, Mizigo, (1977) iliyofanywa na Bi. A. Muro. Tuliangalia kazi hii tafsiri huku tukiilinganisha na kazi asilia, The Burdens ya John Ruganda kwa kuchunguza athari za mtindo katika tafsiri. Tulifanya hivi kwa sababu tuliamini ya kuwa dosari zilizoko katika kazi hii zinajitokeza pia katika kazi zote za fasihi tafsiri. Ni jambo lisilowezekana kuziangalia kazi zote za tafsiri zilizoko katika Kiswahili. Kazi hii tunatumaini ya kuwa itakuwa kielelezo cha yanayohusika katika kitendo cha kutafsiri kazi nyengine za aina hii. . >(tl1lA / I O\T~iri hii irnegawika katika sura nne, kila moja ikijadili kipengele maalumu juu ya kitendo cha kutafsiri kwa mujibu wa fasihi. Kila sura ina hitirnisho ambapo maoni na msirnamo wa tasnifu hii umetolewa kwa mujibu wa yanayojitokeza katika utafiti. Sura ya kwanza ni utangulizi unaobainisha kiini cha utafiti kuhusu sanaa katika tafsiri. Katika sura hii tumeangaza umuhimu wa kufanya uchunguzi kuhusu kitendo cha kutafsiri. Kuna pia madhumuni, misingi ya nadharia, upeo wa tasnifu, sababu za kuchagua somo na jinsi utafiti utakavyofanywa. Sura ya pili inajadili matatizo ya tafsiri kwa jumla na jinsi yanavyochangia katika kupotoka kwa sanaa katika tafsiri. Inaangalia dhana ya tafsiri na kufafanua pamoja na kujadili athari za kila mojawapo ya matatizo hayo kwa sanaa ya makala pokezi. Haya yote yamefanywa kwa ajili ya kuweka misingi thabiti na bora ya uhakiki wa kazi iliyoteuliwa. Sura ya tatu ni uhakiki halisi wa makosa ya kisanaa katika kazi ya Mizigo. Katika sura hii, uhakiki umefanywa kwa mujibu wa misingi ya kinadharia iliyojadiliwa katika sura iliyotangulia. Dosari mbalimbali za kisanaa zinazijitokeza zimetajwa, hali kadhalika matatizo yaliyomkabili mtafsiri. Mambo hayo yote yamechukuliwa rnifano tu ya kuangazia uhalisi wa fasihi tafsiri kwajumla. Sura ya nne ni hitimisho inayotoa muhtasari wa maoni kutokana na utafiti. Maoni ya jumla, mapendekezo ya utafiti mpya na msimamo wa tasnifu umebainishwa.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobi
dc.titleSanaa Katika Tafsiri: Matatizo Na Athari Zakeen
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Artsen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record