Show simple item record

dc.contributor.authorMatundura, Enock S
dc.date.accessioned2013-05-02T06:55:30Z
dc.date.available2013-05-02T06:55:30Z
dc.date.issued2007
dc.identifier.citationTasnifu iliyotolewa iii kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya Master of Arts katika Idaraya Isimu na Lugha, Chuo Kikuu cha Nairobi.en
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18203
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu limekuwa ni kubainisha Jll1S1 taswira dumifu za uana zinavyojitokeza katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Nadharia tete tatu zilizoongoza utafiti huu ni: Mosi, taswira dumifu za uana zinadhihirika katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Pili, wahusika katika fasihi ya Kiswahili ya watoto husawiriwa kwa njia sawa bila kubaguliwa kwa misingi yajinsia zao. Mwisho, waandishi wa kazi za fasihi ya Kiswahili ya watoto huwakilisha idadi sawa ya wahusika wa kike na kiume katika kazi hizo. Kupitia kwa utafiti huu, nadharia tete ya kwanza imethibitishwa kuwa kweli. Lakini nadharia tete ya pili na ya tatu zimethibitishwa kuwa si kweli. Mikabala ya uana na ufeministi ambayo imetumika katika utafiti huu ilitoa msingi madhubuti katika utafiti huu ila tulilazimika kuitumia kwa tahadhari kwa sababu inaakisi mno tamaduni za Kimagharibi. Kuna juhudi zinazofanywa za kutafuta mkabala wa ufeministi unaoafiki zaidi uhakiki wa fasihi ya Kiafrika. Tasnifu hii ina sura tano zinazoshughulikia kipengele cha taswira dumifu za uana katika fasihi ya Kiswahili ya watoto ifuatavyo: Sura ya kwanza inatoa kwa ujumla mwelekeo wa kuchunguza jinsi taswira dumifu za uana zinavyoweza kudhihirishwa katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Inahusisha sehemu kuhusu somo la utafiti, malengo, nadharia tete, sababu za kuchagua somo hili, yaliyoandikwa kuhusu somo hili, msingi wa kinadharia, upeo na mipaka na njia za utafiti. Sura ya pili irnejadili kwa ujumla kuhusu fasihi ya watoto, sifa na majukumu yake. tofauti kati ya dhana 'uana' na jinsia. Aidha sura hii imezungumzia taswira dumifu, Katika sura za tatu na nne, tumechunguza rnatini za tungo za fasihi ya Kiswahili ya watoto za waandishi wa kiume (androtexts) na kike (gynotexts) mtawalia iIi kubainisha jinsi taswira dumifu za uana zinavyojitokeza. Kadhalika katika sura hizi, tumechunguza iwapo wahusika wa kike na kiume wamewakilishwa kwa idadi sawa kwenye matini hizo. Sura ya tano ni hitimisho. Ina sehemu za muhtasari wa matokeo ya utafiti huu kwa misingi ya nadharia tete zilizoongoza uchunguzi huu, matatizo tuliyokumbana nayo katika utafiti huu na mapendekezo kuhusu utafiti zaidi.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobi
dc.titleTaswira Dumifu Za Uana Katlka Fasihi Ya Kiswahili Ya Watotoen
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Artsen


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record