Show simple item record

dc.contributor.authorKarimi, Betty
dc.date.accessioned2013-05-02T08:06:52Z
dc.date.available2013-05-02T08:06:52Z
dc.date.issued2008
dc.identifier.citationMasters Thesis, University of Nairobien
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18267
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia njeo na hali kwa mtazamo wa Uminimalisti. Njeo ill kategoria ya kisarufi inayohusu uhusiano wa kiwakati na hivyo huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo. Hali huangalia jinsi kitendo husika kinavyotendeka sambamba na wakati na hivyo huelezea kuhusu utimilifu na utotimilifu wa kitendo hicho. Madhumuni ya utafiti huu ni kuelezea njeo na hali katika lugha ya Kiswahili na pia kubainisha mofu za kila dhana kwa kuzielezea kwa nadharia ya Uminimalisti. Dhana zote mbili zimeelezewa kwa kina. Mofu za njeo na za hali zimeonyeshwa kwa matumizi ya sentensi mbalimbali. Vielelezo mbalimbali vya nadharia ya Uminimalisti vimetumiwa ili kujaribia kanuni ya ukaguzi wa sifa ya nadharia hii. Katika sura ya kwanza, tumeelezea kwa kifupi kuhusu lugha ya Kiswahili, njeo na hali. Tumeelezea tatizo la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Sura hii pia imeshughulikia sababu za kuchagua mada, upeo wa kazi, msingi wa kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii, njia za utafiti pamoja na umuhimu wa utafiti wenyewe. Aina mbalimbali za vitenzi vya lugha ya Kiswahili zimeshughulikiwa katika sura ya pili. Aidha, mofolojia ya vitenzi hivi imeelezewa na kutambua kuwa mofolojia ya kitenzi husika hutegemea zaidi aina za vitenzi na hivyo mofu zinazopatikana katika kila kitenzi hutegemea aina yake. Katika sura ya tatu,...Qbanaya njeo imeshughulikiwa kwa kina. Dhana ya wakati imeelezewa na ikathibitishwa ni sababu gani njeo haifai kutumiwa kama kisawe cha wakati. Tumeelezea pia dhana ya njeo katika lugha ya Kiswahili Sanifu na kuonyesha mofu anuai zinazowakilisha njeo mbalimbali zinazopatikana katika lugha ya Kiswahili. Sura ya nne imeshughulikia dhana ya hali katika lugha ya Kiswahili. Hali zote zinazopatikana katika lugha hii zimeelezewa na mofu zake kubainishwa. Vielelezo mbalimbali vya nadharia ya Uminimalisti vimetumika. Hitimisho na mapendekezo yametolewa katika sura ya tano. Imebainika wazi kuwa njeo ni tofauti na hali na dhana hizi huhusishwa tu na dhana ya wakati. Lugha ya Kiswahili ina mofu zinazodhihirisha njeo iliyopo, iliyopita na ijayo na vilevile hali timilifu na isiyotimilifu. Mofu hizi hata hivyo huchangiana kimaana kwani zinaweza kutokea pamoja katika sentensi moja. Mofu {na}/{a} hudhihirisha zaidi dhana ya hali isipokuwa pale zinapotumika katika vitenzi vya usemi. Hivyo mofu hizi huonyesha dhana ya njeo na pia ya hali. Nadharia ya Uminimalisti inaweza kuelezea njeo na hali katika lugha ya Kiswahili. Mapendekezo mbalimbali yametolewa katika sehemu ya mwisho.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleNjeo na hall katika lugha ya kiswahili sanifu:Mt azamo wa uminimalistien
dc.typeThesisen
local.publisherSchool of Artsen


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record