dc.description.abstract | Tasnifu hii imehakiki na kutathmini mwingilianomatini katika riwaya mbili za waandishi
tofauti: Rosa Mistika (Kezilahabi) na Tata za Asumini (Ahmed). Tasnifu yenyewe ina
sura tano.
Katika sura ya kwanza tumeshughulikia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia
tete, sababu za kuchagua somo, msingi wa nadharia, up eo na mipaka, yaliyoandikwa
kuhusu mwingilianomatini na aidha njia zilizotumika katika utafiti huu.
Katika sura ya pili tumefafanua istilahi au dhana ambazo hususan hutumika katika
kuhakikia na kutathminia umwingilianomatini. Dhana hizi tumeziita 'vipengele katika
mwanda wa kimwingilianomatini.' Mathalani: wahusika, maudhui, mandhari na aidha
msuko.
Sura ya tatu imejadili mwingilianomatini wa uhusika katika riwaya hizi mbili kwa
kuangazia baadhi ya wahusika na sifa zao. Aidha, sura ya nne imeshughulikia
mwingilianomatini wa kimaudhui. Hapa maudhui ya ujaala, dhuluma dhidi ya
mwanamke, kukata tamaa na aidha malezi yamehakikiwa kwa mujibu wa nadharia ya
umwingilianomatini.
Utafiti wetu umehitimishwa katika sura ya tano. Aidha tumetoa mapendekezo kuhusu
sehemu ambazo zinaweza kufanyiwa tahakiki siku zijazo. | en |