Show simple item record

dc.contributor.authorOrina, B. W. Mong'eri
dc.date.accessioned2013-05-02T08:52:40Z
dc.date.available2013-05-02T08:52:40Z
dc.date.issued2000
dc.identifier.citationMaster of Artsen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18307
dc.description.abstractTasnifu hii ni uhakiki wa utetezi wa maadili katika kazi za kinathari za Shaaban Robert. Tunashughulikia kazi tano peke yake. Uhakiki huu unagawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza tunatoa utangulizi unaohusu wasifu wa Shaaban Robert, na tafsiri ya maadili. Pia tunalieleza tatizo linalotafitiwa; na shabaha za utafiti. Aidha katika sura hii tunatoa sababu zilizotufanya kuchangua mada hii. Hali kadhalika tunataja upeo wa utafiti na kisha tunaeleza msingi wa kinadharia tuliotumia, na pra tunazirejelea kazi zilizoandikwa kuhusu mada tunayoshughulikia, na jinsi tulivyofanya utafiti wetu. Katika sura ya pili, tunatalii aina za maadili katika kazi za kinathari za Shaaban Robert. Mosi tunazungurnzia maadili ya kisiasa kabla ya kuyajadili yale ya kiuchumi na kisiasa. Katika sura ya tatu tunaangalia namna uhusika ulivyotumiwa kuwashilishia utetezi wa maadili. Tunazungurnzia wahusika wa kitaashira wenye matendo merna na maovu. Katika sura ya nne tunatoa mambo matatu yanayoonekana kuwa nguzo muhimu katika utetezi wa maadili. Mambo hayo ni mafunzo, ushujaa na moyo wa subira. Na sura ya tano ina matokeo ya utafiti na utoshelevu wa nadharia tuliyoturnia. Sura hii pia inatoa mapendekezo kwa utafiti zaidi.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobi.en
dc.titleUtetezi wa maadili katika fasihi - nathari va Shaaban Roberten
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Kiswahilien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record