dc.description.abstract | Tasnifu yetu imejishughulisha na maudhui mbalimbali
katika nyimbo za John Mwale.Madhumuni yalikuwa ni
kuangalia mchango wa nyimbo hizi kama aina mojawapo
ya fasihi ya Kiswahili.
Tuna jumla ya sura nne, historia ya mwimbaji na
nyimbo tulizozipitia.
Sura ya kwanza inaelezea mada ya tasnifu historia
fupi ya mwimbaji madhumuni yake, sababu za kulichagua
soma hili, mpaka wa tasnifu, msingi wa nadharia,
yaliyoandikwa kuhusu soma hili na njia za utafiti.
Sura ya pili ni juu ya historia pamoja na miktadha
mbalimbali ya nyimbo, aina ya nyimbo, nyimbo za kazi,
nyimbo za kisasa na hitimisho.
Sura ya tatu ni uchambuzi wa maudhui mbalimbali
katika nyimbo tulizoangalia.
Sura ya nne ni hitimisho pamaja na mapendekezo ya
mhakiki juu ya maswala mbalimbali ya aina ya fasihi
hii. Nyimbo zilizotumiwa zimewekwa mwisho wa tasnifu
hii kama Ambatisho. | en |