Show simple item record

dc.contributor.authorKahiro, Duncan M
dc.date.accessioned2013-05-02T11:36:13Z
dc.date.available2013-05-02T11:36:13Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.citationMaster of Artsen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18367
dc.description.abstractTasnifu hii ni uhakiki wa fani katika tamthilia za Kiswahili ambazo zimetungwa na Wamitila, K.W. Tamthilia hizi ni Wingu La Kupita (1999) na Pango (2003). Katika tahakiki yetu, tumeteua na kujadili vipengele maalum vya fani. Kazi ina sura tano. Katika sura ya kwanza, tumeelezea dhana za kimsingi zinazohusiana au kupatikana katika somo hili. Dhana hizi ni pamoja na: fani na tamthilia. Tumeelezea pia msingi wa kinadharia tulioutumia, sababu za , kuchagua mada hii na upeo na mipaka yake. Tumeweza kurejelea kazi za fasihi zilizowahi kuandikwa zikiangazia fani. Sura ya pili ni kuhusu ujumla na mjengo wa ploti. Katika sura hii tunaeleza dhana ya ploti. Vipengele ambavyo tumejadili ni mfululizo wa vitushi na jinsi vinashirikiana katika kuleta umoja wa kazi na tumetoa tathmini yetu kuhusu ploti katika kila tamthilia. Katika sura ya tatu tumeshughulikia umbuji wa wahusika. Tumejadili jinsi wahusika mbalimbali walivyochorwa katika tamthilia, nafasi au majukumu yao na mchango wanaotoa katika uendelezaji wa kazi. Katika sura ya nne, tumehakiki matumizi ya lugha katika kazi za Wamitila. Tumeangalia jinsi lugha imetumiwa katika mazingira mbalimbali na inavyotumiwa na wahusika wa urnri mbalimbali.Tumejadili pia usanaa na ujumi wa lugha iliyotumiwa. Sura ya tano ni ya hitimisho na mapendekezo. Katika sehemu hii tumeangaza kimukhtasari zile sifa baininifu zinazojidhihirisha katika ujumla wa fani katika kazi za Wamitila kama tulivyoweza kuzijadili na kuzihukumu. Uhakiki wetu umechambua udhaifu au ufanifu wa mtunzi katika umbuji wa wahusika na lugha. Tumeweza kutoa mapendekezo katika tasnifu kuhusu kazi tuliyoifanya.en
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUhakiki wa fani katika tamthilia za K.W. Wamitilaen
dc.typeThesisen
local.publisherFaculty of Arts Kiswahilien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record