dc.contributor.author | Gicheru, Dominic K | |
dc.date.accessioned | 2013-05-03T14:07:13Z | |
dc.date.available | 2013-05-03T14:07:13Z | |
dc.date.issued | 1999 | |
dc.identifier.citation | M.A (Swahili) 1999 Thesis | en |
dc.identifier.uri | http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18795 | |
dc.description | Master of Arts Thesis | en |
dc.description.abstract | Katika tasnifu hii tumelinganisha muundo wa Kikundi Nomino cha Kiswahili Sanifu
na ule wa Kikuyu cha Kabete huku tukionyesha kufanana na kutofautiana kwake.
Hivyo basi tasnifu hii imejikita katika Isimu Linganishi.
Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambamo kumejadiliwa mambo kama;
Somo la utafiti, maelezo mafupi kuhusu lahaja ya Kikuyu cha Kabete (KK) na
Kiswahili Sanifu (KS), madhumuni ya somo tunaloshughulikia, upeo wa somo la
utafiti, mipaka ya somo la utafiti pamoja na yale yaliyoandikwa kuhusu somo hili. Pia
katika sura hiyo tumezitoa sababu zetu za kuamua kushughulikia somo hili,
haipothesia zetu, msingi wa nadharia, pamoja na njia za kufanyia utafiti.
Sura ya pili inashughulikia aina za nomino zinazopatikana katika KS na KK pamoja
na kufafanua ya nomino hizo kwa njia ya kiulinganisho.
Katika sura ya tatu, tumelinganisha muundo wa vipashio vya Kikundi Nomino katika
lugha hizi mbili huku tukifafanua na kulinganisha sheria za kiisimu zinazotawala
muundo wa vipashio hivyo.
Katika ya nne tumejadili kwa undani upatanisho wa kisarufi katika KN cha KS na cha
KK kwa njia ya kiulinganisho. Pia tumejadili upatanisho wa kisarufi kati ya KN na
KT katika sentensi sahili za KK na KS. Mwisho tumeangalia suala la toni kwa kifupi
katika lugha hizi.
Katika sura ya tano tumehitimisha kazi hii huku tukitoa mapendekezo kwa watafiti wa
siku zijazo. | en |
dc.description.sponsorship | University of Nairobi | en |
dc.language.iso | en | en |
dc.title | Ulinganisho wa muundo wa kikundi nomino cha kiswahili sanifu na wacha Kikuyu cha Kabete. | en |
dc.type | Thesis | en |
local.publisher | Depatment of Linguistics, University of Nairobi | en |