Show simple item record

dc.contributor.authorLikhako, Pamela Imbuhila
dc.date.accessioned2013-05-06T06:39:26Z
dc.date.available2013-05-06T06:39:26Z
dc.date.issued1991
dc.identifier.citationM.A (Swahili) 1991 Thesisen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/19234
dc.descriptionMaster of Arts Thesisen
dc.description.abstractKatika tasnifu hii, tumechunguza ufaaji wa Kiswahili kama lugha ya kufunzia katika viwango vyote vya elimu. Tumechunguza utoshelezaji wa Kiswahili katika kufunza hasa masomo ya Kisayansi na taaluma za kiufundi. Tumezingatia hasa Istilahi zilizoko katika masomo ya sayansi na ya kiufundi katika viwango vyote vya elimu na utoshelezaji wa hizi istilahi. Tasnifu hii imeonyesha kwamba Kiswahili kinatosheleza na kinafaa kama lugha ya kisomo. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni dibaji inayotanguliza kazi hii. Katika sura hii tumeeleza mada ya somo letu la utafiti na madhumuni ya tasnifu hiyo. Ni katika sura hii ambapo tunazijadili sababu za kuchagua somo hili, mipaka ya tasnifu hii na msingi wa nadharia tuliyotegemea katika utafiti wetu. Aidha tumejadili kazi za watu mbali mbali waliochunguza kazi inayohusiana na yetu na tukadokeza. na haipothesia zetu. Tumeihitimisha kazi hii kwa kuzieleza njia tulizozitumia katika utafiti huu. Katika sura ya pili, tumejadili hali ya lugha nchini Kenya. Tumejaribu kujadili sababu zinazofanya hali ya lugha kuwa ilivyo. Tumeangalia mfumo wa elimu ya 8.4.4 na athari zake hasa kwa lugha ya Kiswahili. Ni katika sura hii ambapo tumejadili lugha ya sayansi na pia kuchunguza sababu za kudhania kwamba Kiswahili chafaa kama lugha ya kisomo. Katika sura ya tatu tumegusia mashirika na watu mbalimbali wanaoshughulikia uundaji wa istilahi. Pia tumezungumzia njia zinazotumika kuundia istilahi na tukachunguza ubora na udhaifu wa kila njia. Katika sura ya Nne tulijishughulisha na kuchunguza istilahi zilizopo katika masomo tuliyoyachagua ya Kisayansi na ufundi katika viwango mbalimbali vya elimu yaani katika elimu ya msingi, elimu ya upili na elimu ya vyuo. Su~a ya tano ni hitimisho pamoja na kuchunguza matatizo yanayokikumba Kiswahili nchini Kenya.en
dc.description.sponsorshipUniversity of Nairobien
dc.language.isootheren
dc.titleUfaaji wa Kiswahili kama lugha ya kisomoen
dc.typeThesisen
local.publisherDepatment of Linguistics, University of Nairobien


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record