Show simple item record

dc.contributor.authorOng'ondi, Bogonko E
dc.date.accessioned2013-05-06T08:56:43Z
dc.date.available2013-05-06T08:56:43Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.citationM.A (Swahili) 2005 Thesisen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/19323
dc.descriptionMaster of Arts Thesisen
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia uhakiki na unakidi wa riwaya ya Walenisi iliyoandikwa na marehemuMkangi na kutolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa tisaini na tano (1995). Kazihii tumeigawa katika sura sita. Katika sura ya kwanza, tumeweka wazi pendekezo la utafitikwa kuonyesha tatizo la utafiti, sababu za utafiti wenyewe, nadharia tete, msingi wakinadharia na mbinu za utafiti. Vilevile tumeshughulikia upeo na mipaka ya utafiti huu miongoni mwa vipengee vingine vya pendekezo. Sura ya piliinahusu mtazamo kama kipengee mojawapo cha usimulizi. Katikasura hii tumejadili na kuweka wazi maana ya mtazamo na kuonyesha tofauti baina ya mtazamo na usimulizi. Kadhalika, tumeshughulikia sawia mbalimbali za usimulizi katika riwaya ya Walenisi. Vilevile tumeonyesha aina za usimulizi najinsi zinavyodhihirika katika riwaya hii. Katika sura ya tatu, tumeshughulikia unenaji na fikira kama kipengee cha usimulizi. Tumejadili aina tofauti tofauti za unenaji na fikira na kutoa mifano ya kudhihirika kwao katika riwaya hii. Nayo sura ya nne, inaangazia wakati kama kipengeekimojawapo cha usimulizi. Katika sura hii, tumejadili maana ya wakati na umuhimu wake katika usmulizi. Pia tumeonyesha jinsi mbalimbali wakati hudhihirika katika hadithi. Katika sura ya tano, tumejadili mpangilio na uwasilishaji kama.kipengee cha usimulizi. Tumeonyesha wazi kuwa hadithi inaweza kuwa na mpangilio wa moja kwa moja au iwe na mpangilio changamano ambapo kuna uegemezaji. Katika riwaya hii kuna mtindo changamano amhapo tumeonyesha na kufafanua ni kwa nini Mkangi akatumia mtindo huu. Vile vile, katika sura hii, tumeonyesha jinsi hadithi ya Walenisi imewasilishwa ambapo kuna mimesia na daigesia kama mbinu za uwasilishaji hadithi. Tumehitisha katika sura ya sita kwa kurejelea tuliyoyajadili katika sura zote za awali kwa muhtasari tu. Kadhalika tumeelezea matokeo ya utafiti wetu pamoja na matatizo tuliyokumbana nayo tukifanya utafiti huu. Hatimaye tumetoa mapendekezo kuhusu mtalaa huu.en
dc.description.sponsorshipUniversity of Nairobien
dc.language.isootheren
dc.titleUhakiki wa usimulizi katika riwaya ya Walenisi ya Katama Mkangien
dc.typeThesisen
local.publisherDepatment of Linguistics, University of Nairobien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record