Show simple item record

dc.contributor.authorMwangi, Patrick I
dc.date.accessioned2013-05-06T09:24:56Z
dc.date.available2013-05-06T09:24:56Z
dc.date.issued1996
dc.identifier.citationM.A (Swahili) 1996 Thesisen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/19341
dc.descriptionMaster of Arts Thesisen
dc.description.abstractTasnifu yetu imejengwakatika msingi unaoafiki kuwa kamusi za lugha mbilini kazi halisi za tafsiri. Tahakiki nyingiambazo tayari zimeandikwa kuhusu matatizo ya tafsiri zimeegemeazaidikatika fasihi na kazi za kidini. Sisi tunaonyesha kuwa hata kamusi za lugha mbili zina matatizo mengiya tafsiri katika ngazi mbalimbali za lugha. Tasnifu yenyeweimegawanywakatika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumelifafanua somo letu la utaflti ambalo ni leksikografia-tafsiri. Pia, tumeonyesha madhumuni yetu katika utafiti huu na sababu zilizotufanya tuchague somo hili. Fauka ya haya, tumeelezea upeo na mipaka ya tasnifu yetu na pia yaleyaliyoandikwa kuhusu somohili. Tumefafanua pia mwongozowa utafiti wetu na nadharia tete. Mwisho,tumeeleza njia tutakazozitumia katika utafiti wetu. Katika sura ya pili,tumeifafanua dhana ya tafsiri huku tukionyesha matatizo, umuhimu na nafasi yake. Aidha, tumeifafanua dhana ya leksikografia ambapo tumeeleza maana ya kamusi, mambo muhimu katika kamusi na aina za kamusi. Hatimaye tumeifafanua dhana ya leksikografia- tafsiri huku tukionyesha wale ambao hunufaisha na kamusi zalugha mbili. Mwisho,tumeonyesha nafasi ya maana katika tafsiri ya moja kwa moja, tafsiri-huru na tafsirimawasiliano. Sura ya tatu inahusu mambo ya sarufl katika kamusi za uwililugha. Tumeonyesha aina za sarufi, kisha tumefafanua kuhusu matatizo ya kifonolojiakatika kamusi zauwililugha na pia yaleya kimofolojiana kisintaksi. Hatimaye, tumetoa mifanoya tafsiri zisizosahihi kimofolojia na kisintaksi katika kamusi ya Johnson (1939)ya KingerezaKiswahiliambayo tunaitathmini. Sura ya nne ndiyo kiini c}?-akaziyetu. Tumeijadili ,dhana ya semantiki, maana katika semantiki na pia matatizo ya kisemantiki katika kamusi za uwililugha. Matatizo haya yanahusu uchaguzi wavisawe, uchanganuzi wa maana, maneno yajarnii rnojana ufafanuzi wa kimichoro na kimifano. Hatimaye tumeyaonyesha matatizo hayo kama yalivyojitokezakatika kamusi ya F.Johnson (1939). Tumeonyesha pia makosa ya kisemantiki katika mifano iliyotolewana mtunzi na matatizo mengineyajumla katika kamusi hiyo. Sura ya tano ni hitimisho. Tumeonyesha kwakifupiyaletuliyoyashughulikia, yaliyojitokeza kuhusu nadharia-tete, ufaaji wa mwongozo wetu wa utafiti, matatizo tuliyoyapata na kisha tunatoa mapendekezo yetu.en
dc.description.sponsorshipUniversity of Nairobien
dc.language.isootheren
dc.titleMatatizo ya Leksikografia tafsiri: Tathmini ya Kamusi ya F. Johnson (1939)en
dc.typeThesisen
local.publisherDepatment of Linguistics, University of Nairobien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record