Show simple item record

dc.contributor.authorMurage, Joyce N
dc.date.accessioned2012-11-13T12:28:48Z
dc.date.available2012-11-13T12:28:48Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/3313
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu uhakiki wa fani katika Utendi wa Mwana Ninga. Nakala tunayotumia ni ya H.E Lambert katika (Bulletin No.23 of the East African Inter-territorial Language Committee). Utendi huu unaaminiwa kuwa ulitungwa na Furno Liyongo katika mwaka wa 1517. Tunatumia nadharia ya Umuundo. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Katika sura ya kwanza, tumejadili masuala ya utangulizi wa utafiti. Turnezungumzia tatizo la utafiti, madhurnuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na njia za utafiti. Katika sura ya pili, tumejadili misingi ya uhakiki wa fani. Turneeleza maana ya fani na kutoa vipengele vyake mbalimbali.' Pia tumeeleza kuwa tunashughulikia vipengele vifuatavyo katika Utendi wa Mwana Ninga: Ploti, muundo, mandhari, wahusika, usimulizi, toni na matumizi ya lugha. Katika sura ya tatu, tumehakiki ploti na muundo wa Utendi wa Mwana Ninga. Turnebaini kuwa msuko au ploti ya utendi huu ni sahili. Msuko huu ni wa moja kwa moja na unaeleweka kwa urahisi. Pia tumeona kuwa muundo wa utendi huu unafuata kaida za utunzi wa tenzi. Katika sura ya nne, tumehakiki mandhari na wahusika katika Utendi wa Mwana Ninga. Turneona kuwa mandhari ni ya Uswahilini na pia Uarabuni. Pia ni mandhari ya baharini na msituni. Vilevile, tumeona kuwa wahusika ni wawili: Furno Liyongo na Mwana Ninga. Katika sura ya tano, tumehakiki matumizi ya lugha, toni na usimulizi katika Utendi wa Mwana Ninga. Tumeangalia smatumizi ya uhuru wa mshairi na tamathali za usemi. Turneona kuwa tamathali za usemi zinazotumiwa zinaingiliana na mandhari na vilevile sifa za urembo ambazo mtunzi anazisimuli. Kutokana na matumizi ya lugha, tumeona kuwa toni ya utendi huu ni ya mapenzi, furaha matumaini na imani. Usimulizi umetawaliwa na nafsi ya tatu, umoja Tumeona kuwa mtunzi amefaulu katika matumizi ya fani na kutunga utendi wenye mshikamano. Katika sura ya sita na ya mwisho, tunatoa hitimisho na mapendekezo mbalimbali ya utafiti zaidi. Kutokana na utafiti huu tumebaini kuwa vipengele mbalimbali vya fani vinavyotumiwa katika Utendi wa Mwana Ninga vimeingiliana na kuhusiana katika ujenzi wa umbo na muundo wa utendi wenyewe na vilevile kuwasilisha maana. Mintarafu ya hayo, tunahitimisha kuwa mtunzi wa Utendi wa Mwana Ninga amefaulu katika utunzi wake. Tunapendekeza kuwa utafiti zaidi ufanywe kuhusu kipengele eha usimulizi katika utendi huu. Pia uhakiki zaidi kuhusu fani katika utendi huu unaweza kufanywa kwa kutumia nadharia tofauti.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleUhakiki wa fani katika utendi wa mwana ninga: nadharia ya umuundoen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record