Show simple item record

dc.contributor.authorAchieng', Ogola B
dc.date.accessioned2013-07-01T14:56:32Z
dc.date.available2013-07-01T14:56:32Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.citationM.Aen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/43637
dc.description.abstractKatika tasnifu hii iliyolenga kuzipambanua sifa za kishujaa za Furno Liyongo na Lwanda Magere pamoja na umuhimu wao kwajamii zao, imekuwa najumla ya faslu tano. Katika kila faslu tumeshughulikia masuala na vipengele fulani maalum ambavyo vinaingiliana na kukamilishana. Katika faslu ya kwanza tumeangazia usuli wa tasnifu. Tumetanguliza kwa kutoa fasiri kuhusu dhana ya mashujaa na kutoa mifano ya baadhi ya shujaa duniani. Aidha, tumegusia kijuujuu masuala ya jamii na taasisi ya kishujaa. Tumefafanua somo la utafiti, maswali ya utafiti, madhumuni ya utafiti pamoja na nadharia tete. Pia, tumeeleza sababu za kulichagua somo pamoja na kufafanua nadharia ambazo zitatuongoza katika mchakato mzima wa utafiti wetu na njia za utafiti ambazo tutazitumia kupata data ili kutekeleza madhumuni ya utafiti wetu. Katika faslu ya pili, tumefafanua historia ya Furno Liyongo na Lwanda Magere kwa kuifungamanisha na historia ya jamii zao, Waswahili.na jamii' ya Wajaluo mtawalia. Kwa -; ; sababu majagina hawazuki katika li{~we tupu, tumetoa taswira ya mazingira, yaani mazingira ya kitamaduni (ya kijamii, kisiasa na kiuchumi), hali ya kijamii na kipindi ambacho Lwanda Magere na Furno Liyongo walizuka. Aidha, tumeeleza masuala muhimu katika maisha yao. f Katika faslu ya tatu tumelenga kuzilinganisha sifa za kishujaa za Lwanda Magere na Furno Liyongo. Tumezipambanua sifa hizi kW<1kina huku tukionyesha kiwango cha kufanana na kutofautiana kwa sifa hizi. Katika faslu ya nne tumejikita katika ufafanuzi wa umuhimu wa Furno Liyongo na Lwanda Magere kwa jamii zao. Ni katika faslu hii ambapo tumerejelea "taasisi ya shujaa" kama mojawapo ya taasisi nyingi katika mfumo wa jamii yoyote ile na taasisi ambayo huzuka ili ", kutekeleza mahitaji fulani katika jamii. Katika harakati za mashujaa kutimiza mahitaji haya, ndipo umuhimu wao umedhihirika. Katika faslu ya tano tumejumlisha hitimisho ya tasnifu na mapendekezo kuhusu utafiti wa ziada na wa baadaye. Tumeangazia masuala ya kijumla na haswa yanayohusu matokeo ya utafiti wetu. Aidha, tumependekeza baadhi ya masuala ambayo watafiti wa baadaye wataweza kuyamulika.en
dc.description.sponsorshipUniversity of Nairobien
dc.language.isootheren
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleSifa Za Mashujaa Na Umuhimu Wao Kwa Jamii Zao: Ulinganifu Wa Fumo Liyongo Na Lwanda Magereen
dc.typeThesisen
local.publisherFaculty of Arts, University of Nairobien


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record