Show simple item record

dc.contributor.authorToo, Margaret C
dc.date.accessioned2012-11-13T12:32:24Z
dc.date.available2012-11-13T12:32:24Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/4376
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia tamathali za usemi na mbinu nyingine za lugha. Tena tumeziangalia fani za fasihi simulizi ambazo mtunzi wa kazi hii amezitumia na kisha tumelishughulikia suala la wahusika na uhusika wao katika Nguzo Mama (1982). Uchanganuzi wenyewe umezingatia mtazamo wa kafani katika fasihi. Tumeigawa kazi hii katika sura tano. Maarifa yetu ya kitaaluma imejikita kwenye nadharia ya umuundc na semiotiki. Katika sura ya kwanza tumeshughulikia mambo yafuatayo: utangulizi kuhusu mada ambayo imeshughulikiwa, tatizo la utafiti, sababu za kuchagua somo, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, upeo na mipaka na kisha tutangalia mbinu za utafiti wa kazi yetu. Sura ya pili tumeshughulikia tamathali za usemi na mbinu nyingine za lugha zinazopatikana katika Nguzo'Mama. Katika kushughulikia tamathali za usemi, mambo yaliyoangaliwa ni tamathali za maneno, rasamu za sentensi , na kisauti, na tamathali za tafikira kuhusu mbinu nyingine za Iugha. Mambo yatakayoshughulikiwa ni takriri, uzungumzinafsia, kuchanganya ndimi, matumizi ya hotuba na matumizi ya barua katika sura hii. Katika sura ya tatu tumejishughulisha na kuzitambua fani za fasihi simulizi ambazo katika kusawiri mafanikio na matatizo yanayowakabili kina mama, mtunzi amezitumia iii kuufanya mchezo uwe wa kusisimua na kuvutia. Fani hizo zikiwa nyimbo, visakale yaani kuhusu tukio na visa vingine, masimulizi, ngomezi, maigizo, semi na methali. Sura ya nne nayo itashughulikia uchambuzi wa wahusika na uhusika wao. Itaangalia dhana ya mhusika, usawiri wao, na dhima au uamilifu wao katika Nguzo Mama. Mwisho sura ya tano ni mukhtasari na mapendekezo ambayo yanahusu masuala ambayo yatashughulikiwa katika tafiti zitakazofanywa katika siku za usoni.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleUchanganuzi wa kifasihi wa baadhi ya fani katika nguzo mama:mtazamo wa umuundo na semiotikien_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record