Show simple item record

dc.contributor.authorWatuha, Andrew I
dc.date.accessioned2012-11-13T12:32:56Z
dc.date.available2012-11-13T12:32:56Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/4563
dc.description.abstractMadhumuni ya utafiti huu ni kuchunguza na kubaini wazi maudhui ya waadhi katika Utenzi wa Adili ulioandikwa na Shaaban Robert. Maudhui ya waadhi ni wasia au ushauri mbalimbali wa kipekee, katika mazingira mbalimbali, anaopewa mtu ili kumwongoza maishani mwake. Tumeibawibu tasnifu hii katika sura tano. Katika Sura ya Kwanza tumeonyesha tatizo la utafiti. Hali kadhalika tumeeleza lengo la utafiti huu, sababu za kuchagua mada hii, upeo na mipaka ya utafiti, nadharia tete, msingi wa kinadharia na njia za utafiti. Katika kazi hii tumetumia nadharia ya maadili kwa sababu utenzi huu wa Adili una maudhui kemkem ya kiuelekezi kwa kijana wa kiume katika jamii. Kijana Adili, katika utenzi tuliouchanganua, ni kielelezo cha vijana wengine ulimwenguni. Sura ya Pili inaelezea falsafa ya mshairi Shaaban Robert kuhusu maisha kijumla kwa kurejelea baadhi ya dhamira mahsusi katika maandishi yake. Tumeianza sura hii kwa kuelezea maisha ya Shaaban Robert. Vile vile tumeshughulikia mtazamo wake kuhusu maisha. Hapa tumeonyesha jinsi dini na maadili vilivyomwathiri mwandishi pakubwa katika Utenzi wa Adili. Aidha tumemwangalia Shaaban Robert kama mwandishi maarufu na mstahiki. Katika Sura ya Tatu tumechanganua maudhui aina aina ya waadhi ambayo Shaaban Robert alimtongolea kijana Adili kwa kurejelea kikamilifu Utenzi wa Adili.Sura ya Nne inashughulikia baadhi ya vipengele muhimu vya fani vilivyosaidia katika kuwasilisha maudhui ya waadhi. Sura ya Tano ni hitimisho. Katika sura hit tumetoa maoni kuhusu tasnifu hit, matatizo yaliyotokea wakati wa utafiti pamoja na mapendekezo ya kufanywa kwa utafiti zaidi.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleMaudhui ya waadhi katika utenzi wa adilien_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record