Show simple item record

dc.contributor.authorNdung'u, Mary N
dc.date.accessioned2012-11-13T12:35:52Z
dc.date.available2012-11-13T12:35:52Z
dc.date.issued2009
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/5223
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Tumechunguza na kuchanganua tungo ambazo hutambulisha mada na fokasi huku tukitolea maelezo na ufafanuzi wa kina. Malengo ya utafiti huu ni kuchunguza ikiwa kuna uhusiano kati ya mada na fokasi. Pia tumechunguza utambulishaji wa mada na fokasi huku tukitathmini ikiwa mada na fokasi huweza kutambulishwa kwenye kirai. kishazi au kileksika. Mwisho tumetathmini kufanikiwa kwa Mtazamo wa Muundo wa Taarifa katika utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Nadharia ambayo imetuongoza katika utafiti huu ni Mtazamo wa Muundo wa Taarifa iliyoasisiwa na Wanaisimu wa Shule ya Prague. ikaendelezwa na Halliday (1967) na baadaye kukuzwa zaidi na Lambrecht (1994). Muundo wa taarifa husimbwa katika sentensi katika utambulishaji wa mada na fokasi iii kubainisha ni sehemu gani ya sentensi inayobeba taarifa mpya na ni sehemu gani inayobeba taarifa inayojulikana. Katika uchanganuzi wa data. tumeteua data kutoka riwaya ya Kuli ya Adam Shafi (1979) ambayo tumetumia kama data ya kimsingi. Aidha tumepata data zaidi kutoka makaia mbalimbali zilizochapishwa. Zaidi ya hayo tumezalisha data iIi kukidhi mahitaji yetu katika uchanganuzi wa tungo ambazo hutambulisha mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti huu. Imejumlisha utangulizi. mada ya utafiti. madhumuni ya utafiti. nadharia tete. sababu za kuchagua mada hii. upeo na mipaka. uhalalishaji, msingi wa kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti na mbinu za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia maswala ya kimsingi yanayohusiana na mada. fokasi na msingi wa kinadharia wa Muundo wa Taarifa, Katika sura ya tatu. tumeshughulikia na kuchanganua tun go ambazo hutambulisha mada. Tumepata kuwa mada katika sentensi huhitaji kuakisiwa kama vile katika kuitanguliza katika sentensi. kuihamisha kushoto rniongonimwa njia zingine. Katika sura ya tano. tumeangalia jinsi mada na fokasi huhusiana katika muktadha wa utarnbuzi, uchochezi. na ulinganuzi. Tumepata kuwa mpangilio wa maneno katika sentensi huwa na mchango mkubwa katika utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu ambao huwa huru kwa kiasi. Sura ya sita inabeba hitimisho na mapendekezo ya utafiti huu. Katika hitimisho tumetoa rnatokeo ya utafiti yanayohusiana na utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Mapendekezo ambayo tumetoa yatachochea tafiti zaidi katika uwanja huu. Tumependekeza kuwa tafiti zaidi zifanywe katika uchanganuzi wa data wa kimofosintaksia katika utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Pia tafiti zaidi ambazo zitaongozwa na nadharia tofauti au utafiti katika usimbaji wa muundo wa taarifa kwenye tungo changamani za kimofosintaksia au za kiarudhien_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleMada na fokasi katika Kiswahili sanifu: mtazamo wa muundo wa taarifaen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record