Show simple item record

dc.contributor.authorGitonga, Josephat John
dc.date.accessioned2012-11-13T12:36:06Z
dc.date.available2012-11-13T12:36:06Z
dc.date.issued2009
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/5297
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia mabadiliko kimaudhui ya nyimbo za jando za jamii ya Waembu kabla na baada ya ukoloni. Tumetumia mtazamo wa ethnografia haswa kipengele cha ethnografia ya mawasiliano. Kadiri hali ya maisha inavyoendelea kubadilika, ndivyo nayo fasihi simulizi inavyobadilika. Madhumuni ya utafiti huu ni kubainisha kwamba maudhui ya nyimbo za jando haswa za jamii ya Waembu yamebadilika. Maudhui haya yamebainishwa katika vipindi viwili bainifu ambavyo ni kabla na baada ya ukoloni. Vipindi hivi viwili vinaangazia hali mbili za kimaisha. Kabla ya ukoloni, maisha yalikuwa tofauti na hivyo basi maudhui ya nyimbo hizi yalikuwa tofauti. Baada ya ukoloni, maisha yalibadilika na kwa hivyo kusababisha kubadilika kwa maudhui ya nyimbo hizi. Katika sura ya kwanza, tumeeleza kwa kifupi kuhusu nyimbo kwa jumla. Tumeeleza tatizo la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Sura hii pia imeshughulikia sababu za kuchagua mada, upeo wa utafiti, msingi wa kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na njia za utafiti. katika sura ya pili tumeshughulikia maana ya fasihi kwa jumla, fasihi simulizi na historiaya jamii ya Waembu. Pia vipindi hivi viwili ambavyo jamii hii ilivipitia vimeelezewa. Katika sura ya tatu tumebainisha maudhui ya fasihi simulizi kwa jumla. Vilevile tumeelezea maudhui ya nyimbo za jando za Waembu kabla ya ukoloni. Tumeelezea maudhui ya nyimbo hizi baada ya ukoloni huku tukibainisha mabadiliko yake. Hitimisho na mapendekezo yametolewa katika sura ya nne. Imebainika wazi kuwa baadhi ya maudhui ya nyimbo hizi yamebadilika kiwakati katika nyimbo hizi. Mapendekezo mbalimbali yametolewa katika sehemu ya mwisho. Nyimbo za jando za jamii hii ambazo zimeandikwa kwa lugha ya Kiembu na kutafsiriwa katika lugha ya Kiswahili zimo katika viambatisho.Vilevile ramani ya wilaya ya Embu imo katika sehemu hii.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleMabadiliko kimaudhui ya nyimbo za jando za jamii ya waembu: kabla na baada ya ukolonien_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record