dc.description.abstract | Tasnifu hii inahakiki ujagina wa mwanamke katika Pango. Mwongozo wetu katika kazi
hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Inalenga kuibua ujagina wa mwanamke katika
jamii inayoongozwa na mfumo kandamizi wa ki-ubabedume. Tumeigawa kazi hii katika
sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti,
nadharia tete, sababu ya kuchagua mada ya utafiti, upeo na mipaka ya tasnifu, msingi wa
nadharia, yalioandikwa kuhusu somo hili na hatimaye njia za utafiti. Sura ya pili
imeshughulikia ujagina wa mwanamke na asasi za jamii. Asasi hizi tukasema ni pamoja
na dini, ndoa na elimu. Sura ya tatu inahusu ujagina wa mwanamke unavyodhihirika
katika Pango. Sura ya nne imeshughulikia wahusika wengine wanavyochangia ujagina
wa mwanamke katika Pango. Hatimaye sura ya tano ni hitimisho ambapo muhtasari wa
matoke ya utafiti, mapendekezo pamoja na tafiti za baadaye zimeshughulikiwa. | en |