Show simple item record

dc.contributor.authorNjue, Caroline W
dc.date.accessioned2012-11-13T12:37:56Z
dc.date.available2012-11-13T12:37:56Z
dc.date.issued2010
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/5896
dc.description.abstractUtafiti huu umeshugulikia uchanganuzi wa proposisheni katika Kiswahili. Tumetumia Nadharia ya Uhusiano ya Sperber, D na Wilson, D. (2003), haswa vipengee vyake ambavyo ni; kanuni ya mawasiliano katika uhusiano na kanuni ya utambuzi katika uhusiano. Madhumuni ya utafiti huu ni kubainisha kuwa dhana hii ya proposisheni ina maana katika pragmatiki kwa sababu proposisheni imechunguzwa katika nyanja za semantiki. Vilevile, proposisheni hubainika na kueleweka vyema hasa inapohusishwa na muktadha. Hivyo basi, tumebainisha ufahamu huu kwa kutumia miktadha tofauti. Katika sura ya kwanza; tumeeleza kwa kifupi kuhusu proposisheni kwa jumla. Tumeeleza tatizo la utafiti na kuorodhesha madhumuni na nadharia tete za utafiti huu. Sura hii pia imeshugulikia sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka katika utafiti, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na njia za utafiti. Katika sura ya pili, tumeshugulikia dhana ya proposisheni katika undani, aina tofauti za proposisheni, ishara za proposisheni nzuri. Vilevile, katika sura hii tumejihusisha na maana ya kiproposisheni iliyoko katika sentensi na proposisheni katika sentensi mbalimbali. Katika sura ya tatu, tumeshughulikia proposisheni na istilahi nyingine, proposisheni katika vitendo usemi; lokusheni, ilokusheni na palokusheni. Vilevile, katika sura hii tumejihusisha na proposisheni katika chukulizi na umaanisho, proposisheni katika miktadha tofauti na proposisheni katika semantiki na pragmatiki. Katika sura ya nne, tumejihusisha na uchanganuzi wa data, mfanyiko uliopo katika kuufasiri ujumbe, uzalizaji wa proposisheni. Pia, katika sura hii tumejihusisha najukumu la muktadha kwa kufahamu proposisheni katika rnazungurnzo anuwai, rnatarajio katika uhusiano baina ya rnsernaji na msikilizaji. Mwishowe katika sura hii, turnewalinganisha Wilson na Sperber dhidi ya Grice kwa kulinganisha dhana za kirnsingi na kanuni baina yao. Katika sura ya rnwisho ambayo ni ya tano, turneshugulikia rnuhtasari, rnahitirno na mapendekezo. Turneutoa rnuhtasari wa yote tuliyoyajadili katika utafiti huu kutoka sura ya kwanza hadi sura ya tano, kisha kutoa rnapendekezo katika utafiti kwa wakati ujao.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleUchanganuzi wa proposisheni katika Kiswahili: nadharia ya uhusianoen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record