Uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya mpya: babu alipofufuka (said Ahmed Mohamed) na watu wa Gehenna (Tom Olali )
Date
2013-11Author
Mwangi, Jedidah Wanjiru.
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii inahusu uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya za Said Ahmed
Mohammed (Babu Alipofufuka) na Tom Olali (Watu wa Gehenna). Katika utafiti
huu tumechunguza uhalisiajabu katika kiwango cha wahusika na mandhari katika
riwaya hizi teule tukiongozwa na nadharia ya uhalisiajabu. Ili kufikia malengo
yetu, utafiti huu umegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza,
tumetanguliza mada yetu, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete,
msingi wa nadharia, yalioyoandikwa kuhusu mada yetu, na njia za utafiti.
Katika sura ya pili, tumechunguza hatua za mwanzo za uhalisiajabu ambazo ni
uhalisia hakiki, uhalisia wa kijamaa hadi kufikia uhalisiajabu. Tumetambua ya
kwamba waandishi waliotumia uhalisia kama vile Said A. Mohammed na K.W.
Wamitila wamegeukia mtindo wa uhalisiajabu ili waweze kuyazungumzia mambo
ambayo hawangeweza kuweka wazi kwa mtindo wa uhalisia.
Katika sura ya tatu, tumechunguza na kubainisha vipengele vya uhalisiajabu
katika viwango vya wahusika na mandhari yenye matukio ya uhalisia na
uhalisiajabu katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Katika sura ya nne, tumebainisha
wahusika na mandhari yenye matukio ya uhalisia na uhalisiajabu katika riwaya
ya Watu wa Gehenna.
Katika sura ya tano, tumetathmini matokeo ya uchunguzi wetu kwa kurejelea
madhumuni na nadharia tete zetu. Tumetoa hitimisho na mapendekezo ya utafiti
wa baadaye.
Citation
Tasnifu Hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Shahada Ya Uzamili Katika Idara Ya Isimu Na Lugha, Chuo Kikuu Cha NairobiPublisher
University of Nairobi Department of Linguistics and Languages