Sintaksia ya kijalizo cha Kiswahili Sanifu: mtazamo wa x-baa.
View/ Open
Date
2013-10Author
Koech, Lily C
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti wetu umechanganua kijalizo cha Kiswahili kwa kutumia nadharia ya X-baa.
Tumepanua tafsiri ya kijalizo cha Kiswahili sanifu na kubainisha uamilifu wake katika tungo.
Tumebainisha miundo tofauti ya vijalizo na kudhihirisha sheria zinazotawala uunganishwaji
wa vipashio vinavyojaliza virai tofauti katika sentensi.
Sura ya kwanza inaweka wazi mada ya utafiti, sababu ya kuchagua somo, madhumuni ya
utafiti, nadharia tete, msingi wa kinadharia na yaliyoandikwa kuhusu mada.
Katika sura ya pili tumewekea msingi kazi yetu kwa kufafanua dhana tofauti ambazo
tumetumia katika kuchanganua kijalizo. Dhana hizi ni kama vile, sintaksia, vishazi, virai na
kategoria amilifu za sentensi.
Katika sura ya tatu tumechanganua miundo tofauti ya Kijalizo. Kijalizo kinaweza kuwa
nomino au kirai nomino, kihusishi au kirai husishi, kivumishi au kirai vumishi, kitenzi au
kirai tenzi. Pia tumejadili aina tofauti za kijalizo kwa msingi wa nadharia ya x-baa. Kwa
mfano, kijalizo cha kitenzi, kijalizo cha nomino, kijalizo cha kivumishi kijalizo cha kihusishi
na kile cha kielezi.
Katika sura ya nne, tumeandika matokeo ya utafiti, mapendekezo na mwisho ,
hitimisho.Tuligundua kuwa dhana ya kijalizo hueleweka kwa njia nyingi kutegemea
mwelekeo wa nadharia inayotumiwa. Kijalizo katika sarufi mapokeo kilichukuliwa kuwa
neno au fungu la maneno linalotokea baada ya kitenzi kishirikishi.
Katika utafiti wetu, tumetumia nadharia ya x-baa kufafanua kijalizo. Kijalizo katika nadharia
ya x-baa ni neno au fungu la maneno linalofungamanishwa moja kwa moja na kichwa cha
kirai husika (dada ya kichwa cha kirai). Kijalizo hupanua kichwa cha kirai hadi kiwango
vii
kingine. Kwa mfano: Funga huo mlango. Maneno kwenye mlazo ni kijalizo cha kitenzi
‘funga’.
Citation
Shahada Ya Uzamili Ya Kiswahili Katika Chuo Kikuu Cha Nairobi, 2013Publisher
University of Nairobi, IDARA YA KISWAHILI