Show simple item record

dc.contributor.authorNguti, Mary
dc.date.accessioned2013-11-25T15:28:56Z
dc.date.available2013-11-25T15:28:56Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.citationTasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Nairobien
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60185
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulika na kulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha ya Kikamba na ya Kiswahili. Ingawa tasnifu hii imetolewa kwa mahitaji ya shahada ya Kiswahili, data iliyochanganuliwa ni kutoka lugha ya Kikamba na ya Kiswahili. Uchanguzi huu tuliufikia kwa kutambua umuhimu unaostahili kupewa lugha zetu nyingine za Kiafrika katika muktadha wa nyumbani na miktadha mingine mbalimbali. Kwa sababu ya juhudi zinazofanywa na kila jamii kuikuza na kustawisha maadili katika maisha ya binadamu wote (Stockwell, 2008). Ndiposa tukawa na jukumu la kuchunguza matumizi ya tasfida za nyumbani. Somo la tasnifu hii ni ulinganishi wa matumizi ya tasfida katika lugha ya Kikamba na Kiswahili katika muktadha wa nyumbani. Tumechunguza matumizi ya tasfida kwa lugha ya Kikamba na kulinganisha na matumizi katika lugha ya Kiswahili. Hatukulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha hizi mbili kwa kutaka kulingamisha tu bali, kwa kufanya hivyo tumetoa mwanga zaidi kuonyesha kuwa, tasfida ni chombo muhimu na maalum cha mawasiliano katika jamii yoyote. Tumeonyesha kwamba jamii mbili zinazotofautiana kwa mengi huweza kuwa na mawazo sawa kuhusu jamii na mazingira yao kwa jumla. Madhumuni makuu katika tasnifu hii yalikuwa kulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha hizi mbili, Kikamba na Kiswahili ili kudhibitisha kuwa, kunao uhusiano mkubwa katika matumizi ya tasfida. Tumechambua jinsi matumizi ya tasfida hufanikisha mawasiliano katika lugha ya Kikamba na Kiswahili. Tulikuwa na shabaha pia ya kuchunguza jinsi hali za jamii kama umri, Kazi, jinsias na hadhi huathini matumizi ya tasfida. vii Data ilikusanywa kupitia mahojiano na hojaji zilijazwa na watafitiwa wateule. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa na kubainishwa kwa msingi wa nadharia ya Upole iliyoasisiwa na Penelope Brown na Levinson (1978).en
dc.language.isoenen
dc.titleUlinganishi Wa Matumizi Ya Tasfida Za Muktadha Wa Nyumbani Katika Lugha Ya Kikamba Na Kiswahilien
dc.typeThesisen
local.publisherUniversity of Nairobien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record