Ukuaji wa muundo na mawazo katlka tamthilia za Timothy Arege mtazamo wa umuundo
Abstract
Utafiti huu umechunguza ukuaji wa muundo na mawazo katika tamthilia za Timothy
Arege. Tamthilia zilizoteuliwa kuhakikiwa ni tatu. Nazo ni: Cham chela (2007), Kijiba
cha Moyo(2009) na Mstahiki Meya (2011 )
Sura ya kwanza ni utangulizi, tatizo la utafiti, madhumni ya utafiti, nadharia tete, upeo na
mipaka na msingl wa nadharia. Pia, tumejumuhisha yaliyoandikwa kuhusu mada, na
mbinu za utafiti zizotumika katika kazi hii.
Sura ya pili imeshughulikia msuko kama rnojawapo wa vipengele vya muundo na
mchango wake katika tamthilia za Arege. Tumetanguliza kwa kuangazia dhana ya
msuko, kanuni za ploti pamoja na mchango wao katika kuendeleza ukuaji wa muundo na
mawazo katika tamthilia za Arege.
Sura ya tatu imeangazia mchango wa wahusika katika kuendeleza dhamira na maudhui.
Tumeshughulikia majukumu yao na mchango wao katika kuibua maudhui na dhamira.
Sura ya nne nayo imeshughulikia mchango wa matumizi ya lugha katika kudhihirisha
ukuaji wa muundo na mawazo katika tamthilia za Arege. Tumeshughulikia tamathali za
lugha kama vile tashihisi, balagha, uzungumzinafsia, kuchanganya ndimi, tashbihi,
dhihaka, methali, mdokezo, sitiari na kinaya.
Sura ya tano inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti na mapendekezo ya tafiti za
baadaye.
Citation
Ndege Magati Charles (2013). Ukuaji Wa Muundo Na Mawazo Katlka Tamthilia Za Timothyarege Mtazamo Wa Umuundo. Shahada Ya UzamiliPublisher
University of Nairobi