Show simple item record

dc.contributor.authorNjoroge, Anne W
dc.date.accessioned2014-11-25T05:43:45Z
dc.date.available2014-11-25T05:43:45Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/75212
dc.description.abstractKatika utafiti wetu tumeangazia viongozi kama visababishi vya mabadiliko katika riwaya za Vipanya Vya Maabara na Majira Ya Tufani. Jamii mbalimbali huwa na mitazamo anuai kuhusu majukumu ya viongozi na mchango wao hauwezi kupuuzwa. Mwandishi wa riwaya hizi ameangazia majukumu ya viongozi yanayoshabihiana katika kuleta mabadiliko kwenye jamii zake, hivyo basi makala haya yanachunguza mchango wa viongozi kama visababishi vya mabadiliko dhahiri. Tulichagua mada hii ili kuchambua riwaya hizi kwa sababu ya maudhui yanayoashiria jinsi hali halisi ilivyo katika jamii zetu. Malengo ambayo tumeyaangazia ni kuchunguza jinsi matendo ya viongozi yanavyohujumu uchumi wa nchi, kutathmini ikiwa matendo ya viongozi yanaakisi maadili ya kijamii na kupambanua hali za unafiki zinazodhihirika katika matendo ya viongozi. Tulijikita kwenye kazi hizi mbili Vipanya Vya Maabara na Majira ya Tufani pamoja na kurejela kazi zingine ili kutoa idhibati zaidi. Tuliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki Usemi iliyoasisiwa na Norman Fairclough, Teun Van Djik na Ruth Wodak miongoni mwa wengine,kwa mitazamo ya Wodak na Reisigl,inayozingatia mkakati wa kurejelea, mkakati wa unominishaji, mkakati wa ubishi, mkakati wa kudhihirisha nguvu za usemi na vilevile mkabala. Baadhi ya mambo yaliyojitokeza katika utafiti wetu ni kwamba mabadiliko yanayoshuhudiwa katika nchi na jamii mbalimbali husababishwa na viongozi. Kwa mfano ufisadi, utabaka, wizi wa kimabavu, hujuma miongoni mwa maovu mengine mengi. Mabadiliko haya yanasababishwa na kuweko kwa uwezo mkubwa wa watawala katika kuwatawala watawaliwa.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.titleViongozi kama visababishi vya mabadiliko katika riwaya za Mwenda Mbatiah: Vipanyam vya maabara na majira ya tufanien_US
dc.typeThesisen_US
dc.type.materialen_USen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record