dc.description.abstract | Nchini Kenya, walimu wa shule za msingi ni kielelezo cha kuigwa na wanajamii walio wengi
hasa katika maeneo ya mashambani. Aghalabu, wanayoyatenda na wanayoyasema walimu hawa
kuhusiana na lugha ndiyo yanayofuatwa na wanajamii walio wengi. Tasnifu hii ni uchunguzi wa
mielekeo ya wadau hawa muhimu kuhusu majukumu yaliyotengewa lugha mbalimbali, ukuzaji
na uendelezaji wa matumizi ya lugha kama inavyoangaziwa na kauli za Katiba ya Kenya
zihusuzo suala la lugha. Mielekeo ya wadau hawa inatarajiwa kuwa mwongozo kwa waundaji
sera ya lugha na pia wapangaji lugha ili kubuni mikakati ya kuhimiza ushawishi na uhusika wa
walimu husika, kama wadau muhimu, katika kutekeleza sera ya lugha kama inavyojitokeza
katika Katiba ya Kenya ya mwaka wa 2010. Uchunguzi huu ulijikita nyanjani ambapo data
ilikusanywa kwa njia ya hojaji, mahojiano na utazamaji wa tabia za watafitiwa kuhusu lugha ya
Kiswahili, Kiingereza na lugha asilia (Kimeru). Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mielekeo ya
watafitiwa kuhusu suala la lugha kama linavyojitokeza katika Katiba ya Kenya, imetokana na
masiala ya kihistoria, kijamii, kiisimu na kiuchumi. Uchanganuzi wa data ya utafiti huu
uliongozwa na nadharia ya Kijamiinafsia iliyoasisiwa na Lambert (1963) na ile ya Kijamii ya
Fishman (1972). | en_US |