Athari Za Sheng Katika Matokeo Ya Mtihani Wa Kiswahili Katika Shule Za Msingi Mtaa Wa Kangemi
Abstract
Utafiti huu ulihusu Athari za Sheng katika matokeo ya mtihani wa Kiswahili katika shule za
msingi mtaa wa Kangemi. Kazi hii imegawanywa katika sura tano, Katika sura ya kwanza
tumeangazia maswala muhimu ya utafiti wetu. Tumeelezea swala la utafiti, madhumuni na
nadharia tete zilizotuongoza. Aidha, sababu za utafiti, zimeelezwa pamoja na upeo na
mipaka. Mwisho, mbinu za utafiti zimebainishwa na uchanganuzi data kufanywa. Vile vile
katika sura hii tumeweza kuangazia yaliyosemwa kuhusu Sheng na wataalam mbalimbali.
Katika sura ya pili tumeangazia mbinu mbalimbali ambazo wanajamii wa lugha ya Sheng
huzitumia katika kuunda misamiati yao.
Aidha katika sura ya tatu tumeshughulikia nyenzo mbalimbali ambazo wanafunzi wa shule
za msingi hujifunza Sheng kutokana nazo. Sura ya nne nayo tumechanganua data za matokeo
ya mtihani ya Kiswahili ya kitaifa. Utafiti wetu umeweza kuangalia matokeo ya shule nne
katika mtaa wa Kangemi. Sura ya tano ambayo ni ya mwisho, tumejikita katika matokeo ya utafiti, mahitimisho, mambo ibuka pamoja na mapendekezo ya utafiti wa baadaye.
Publisher
University of Nairobi