dc.contributor.author | Njoroge, Florence W | |
dc.date.accessioned | 2014-12-02T11:04:26Z | |
dc.date.available | 2014-12-02T11:04:26Z | |
dc.date.issued | 2014 | |
dc.identifier.citation | (M.A) Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nairobi. | en_US |
dc.identifier.uri | http://hdl.handle.net/11295/75919 | |
dc.description.abstract | Sheng imekuwa moja wapo wa lugha vipindi ambayo inatumika sana kwenye miji mingi
nchini Kenya ukiwemo mji wa Nakuru. Matumizi ya lugha hii nyumbani, mitaani na hata
shuleni umepelea lugha hii kukua na hata kuongeza misamiati na kuongezeka kwa
watumiaji wa lugha hii. Utafiti huu ulilenga kutambulisha hali, hadhi na majukumu ya
Sheng mjini Nakuru huku tukilinganisha Sheng na lugha nyingine zinazotumika mjini
humo. Sababu ya kuteua mada hii ni kuona kuwa vijana wengi mijini wanatumia Sheng
kama kitambulisho chao kilugha na haijatambulika kisheria. Malengo ya kazi hii
nikutafiti kama Sheng ina majukumu maalum mjini Nakuru, kama hadhi ya lugha hii ni
ya chini na kama kuna tofauti zilizoko katika matumizi ya Sheng kimaeneo. Ukusanyaji
wa data kwa ajili ya utafiti huu ulifanywa kwa njia ya hojaji ambayo iliyafumbata
maswala ambayo kwa kawaida hupelekea mtuamiaji wa lugha kuonekana kana kwamba
ni mtu aliye na uelewa wa lugha tofauti mbali na kuonyesha hadhi zipewazo lugha mjini
Nakuru. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia nadharia ya lugha na utambulisho
wa jamii ya Gumperz na Cook (1982), nadharia chanzo cha ujifunzaji wa lugha ya pili ya
Stephen Krashen (1989) na nadharia ya jumuishi na utambulisho ya Gile (1979).
Uchanganuzi kutokana na nadharia hizi umeonyesha kuwa kila lugha huhusishwa na
kikundi fulani cha wahusika na lugha hii huwa kama kitambulisho cha jamii husika. Kila
lugha hupewa majukumu na hadhi kulingana na watumizi wake ni kina nani. Mbinu za
ujifunzaji lugha pia huchangia katika kuipa lugha fulani majukumu na hadhi ya lugha
husika. Sheng ni lugha ambayo ni kitambulisho cha vijana wa mijini nchini Kenya
ukiwemo mji wa Nakuru | en_US |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.publisher | University of Nairobi | en_US |
dc.title | Hali, Hadhi Na Majukumu Ya Sheng Mjini Nakuru | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |
dc.type.material | en_US | en_US |