Show simple item record

dc.contributor.authorAmolloh, Shadrack
dc.date.accessioned2013-02-12T14:43:56Z
dc.date.available2013-02-12T14:43:56Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/8123
dc.description.abstractUtafiti huu umejaribu kuhakiki hatua za serikali za kutekeleza sera mpya ya lugha ya matumizi rasmi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika shule za msingi. Sera mpya ya lugha katika utafiti huu ni ile kauli ya Katiba ya Kenya (2010) inayokipa Kiswahili hadhi rasmi. Utafiti umejikita katika kiwango cha maamufi, uratibishaji na usimamizi wa mchakato wa utekelezaji wa sera za kielimu nchini kwa vile sera hii ingali sheria. Tatizo ambalo utafiti huu ulinuia kuchunguza ni He mikakati inayoandaliwa na serikali ili kufanikisha utekelezaji wa sera hii katika mfumo wa elimu hususa kama lugha ya kufundishia katika shule za msingi. Hatua hii ilikusudia kutubainishia changamoto zitakazokumba shughuli ya utekelezaji wa sera mpya ya lugha kama nyenzo ya kufundishia katika ngazi hii ya elimu. Aidha, kutumia matokeo haya, tulikusudia utoa mapendekezo ya jinsi ya kufaulisha utekelezaji lengwa wa sera rejelewa. Data msingi ya utafiti huu ilikusanywa kupitia kwa mahojiano rasmi ya ana kwa ana na wawakilishi wa waunda sera katika Wizara ya Elimu, Wizara ya Haki, Mshikamano wa Kitaifa na Maswala ya Kikatiba na Taasisi ya Elimu Kenya. Tulichagua Wizara hizi na Taasisi hii kwa vile ndizo zenye dhamana ya kuunda, kutoa mwelekeo na kuratibisha utekelezaj i wa sera za kielimu. Aidha, jukumu la ukufunzi wa walimu na vifaa vya kufunzia katika shule za msingi ni wao. Utafiti huu umebainisha kwamba, kufikia sasa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na serikali Hi kuidhinisha matumizi rasmi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika shule za msingi. Kwa hiyo, hakujabuniwa vyombo vinavyotarajiwa kusaidia katika utekelezaji wa sera hii mpya ya lugha. Pia, vifaa vya kufunzia na walimu wa shule za msingi hawaandaliwi kwa njia inayowawezesha kufanikisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya Kufundishia. Isitoshe, serikali ina wahaka kuwa Kiswahili kinaweza kutumiwa kufundishia masomo mengine. Kwaju~la, utafiti wetu umeonyesha changamoto kadhaa ambazo zitatinga ufanisi wa sera mpya ya lugha katika shule za msingi. Tumeziorodhesha katika matapo yafuatayo: changamoto za kielimu, changamoto za kiisimu, changamoto za kiusimamizi na changamoto za kisiasa na kimwelekeo. Katika misingi ya nadhariajumuishi ya utambulisho ya Giles (1979), tumechanganua data na kutoa mapendekezo ya namna tunavyoweza kutekeleza sera hii ya lugha ili Kiswahili kichukue mahali pa Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika shule za msingi. Kwanza, tumependekeza kuundwa kwa taasisi na mashirika ya kitaaluma ambayo mbali na kusaidia katika mchakato wa utekelezaji wa sera hii, pia yatakuwa na jukumu la kusimamia ukuzaji na maendeleo ya Kiswahili nchini. Pili, tumetaja matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kukikuza Kiswahili kiyamudu majukumu ya kielimu. Vilevile, tumehimiza serikali kushirikiana na Tanzania yenye tajiriba ya kukitumia Kiswahili kufundishia shule zao za msingi kwa zaidi ya miaka arubaine. Ni baada ya kufanya hivi ndipo tutakapoweza kuvuna matunda ya kutumia lugha ya kienyeji kama nyenzo ya kutoa maarifa ambayo ni msingi wa maendeleo, vilevile kujenga utamaduni wa taifa ambao ni utambulisho wa jamii.en_US
dc.language.isoOtheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleSera mpya ya lugha nchini Kenya: changamoto za utekelezaji wa matumizi rasmi ya Kiswahili kama lugha ya kufundisha katika shule za msingien_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record