Show simple item record

dc.contributor.authorChisia, Modgen
dc.date.accessioned2013-02-12T14:47:10Z
dc.date.available2013-02-12T14:47:10Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/9090
dc.description.abstractKazi hii inahusu uchanganuzi wa Kauli katika sentensi elekezi ya Kiswahili sanifu kwa kutumia nadharia ya Ubanifu. Kazi yenyewe ilikuwa na malengo ya kueleza dhana ya uambishaji na kuonyesha viambishi vya kauli katika kitenzi cha Kiswahili sanifu. Aidha, kazi hii imelenga kuonyesha uhusiano uliopo kati ya yambwa na viambishi vy'a kauli katika sentensi elekezi ya Kiswahili sanifu. Kazi hii imefaulu katika kuonyesha kuwa dhana za uambishaji na unyambuaji ni taratibu mbili tofauti za kisarufi, na kwamba viambishi vya kauli ni tokeo la uambishaji wala sio la unyambuaji. Utaf'liti huu umebainisha kwamba viambishi vya kauli sio tu viambishi tamati, bali pia huongozwa na kanuni mbalimbali ikiwemo kanuni ya wiano wa irabu. Utafiti huu umeonyesha pia kwamba, Usogezi kama mojawapo ya mihimili mikuu ya nadahria ya Ubanifu, huongozwa na kanuni mbalimbali za iktisadi kwa lengo la kufanikisha ukuaguzi wa sifamuhimu. Kazi yenyewe imepangwa katika sura tano; kila sura ikishughulikia vipengele mahususi. Sura ya kwanza imetoa utangulizi wa jumla kuhusu dhana za kauli na sentensi elekezi. Aidha sura hii imefafanua tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete zilizoongoza utafiti pamoja na kueleza sababu za kuchagua mada ya utafiti. Sura hii pia imebainisha upeo na mipaka ya utafiti kabla ya kufafanua msingi wa nadharia iliyotumiwa ya Ubanifu na kudurusu yaliyoandikwa kuhusu kauli na nadharia ya Ubanifu. Hatimaye, sura hii imeeleza mbinu za utafiti na umuhimu wa utafiti huu. Sura ya pili imeshughulikia dhana za uambishaji na unyambuaji na kutoa vigezo vitano vya kuzitofautisha. Aidha, sura hii imeangazia viambishi awali na tamati vya vitenzi vya Kiswahili sanifu kwa kina. Katika sura ya tatu, vitenzi vya Kiswahili vimefafanuliwa kwa kuonyesha aina zake kwa misingi mitatu. Sura hii imehitimishwa kwa kuangazia kauli mbalimbali za vitenzi vya Kiswahili katika muktadha wa sentensi elekezi. Sura ya nne imejishughulisha na uchanganuzi wa data yetu ambapo kauli tisa za vitenzi zimeelezwa kwa kutumia nadharia ya ubanifu. Dhana za uhusika na valensi pia zimeshughulikiwa hapa. Sura hii imetathmini kwa kina nafasi ya kanuni mbalimbali za nadharia ya Ubanifu zinazohakikisha kuwa tungo zinazozalika zinakuwa sahihi sio tu kifonetiki, bali pia .kimantiki. Sura ya tano ya tasnifu hii imetoa mahitimisho ya utafiti wetu. Zaidi ya mahitimisho, sura hii imetoa mapendekezo ambayo watafiti wengine wanaweza kuzingatia katika tafiti zao za baadaye.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen
dc.titleUchanganuzi Wa Kauli Katika Sentensi Elekezi Ya Kiswahili Sanifu: Mtazamo Wa Nadharia Ya Ubanifuen
dc.typeThesisen


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record