Uhakiki wa usimulizi katika tamthilia ya kijiba cha moyo na mstahiki meya
View/ Open
Date
2015-11Author
Khamis, Biasha S
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu umeshughukilia usimulizi katika tamthilia ya Kijiba cha Moyo na Mstahiki Meya kwa kutumia nadharia ya naratolojia kwa mtazamo wa Genette (1972-1983). Utafiti huu una malengo mawili: Kwanza, kubainisha vipengele vya usimulizi. Pili, kujadili dhima ya vipengele vya usimulizi katika tamthilia za Kijiba cha Moyo na Mstahiki Meya. Vipengele vilivyochunguzwa ni pamoja na kipengele cha wakati, daraja na sauti za usimulizi na wahusika na uhusika. Utafiti huu umeongozwa na nadharia tete zifuatazo: (i) Usimulizi unadhihirika katika tamthilia. (ii) Vipengele vya usimulizi hutekeleza dhima maalum katika tamthilia. Kutokana na utafiti wetu nadharia tete zetu zimethibitika. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa usimulizi upo katika tamthilia na imebainika kuwa vipengele vya usimulizi vina dhima muhimu katika kusimulia hadithi na kupitishia maudhui na dhamira katika tamthilia kama ilivyo katika riwaya na hadithi fupi.
Publisher
University of Nairobi