dc.description.abstract | Nafasi ya fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya
Waswahili na Wataveta ni utafiti wenye gharadhi ya kuonyesha jinsi fani za kiutendi
zinavyotumiwa katika nyimbo zinazoimbwa wakati wa harusi.Tulichokusudia
kufanya katika utafiti wetu ni kulinganisha fani za kiutendi katika nyimbo za harusi
miongoni mwa jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Malengo ambayo tulikusudia
kuangazia ni kubainisha aina mbali mbali za fani za kiutendi,kuonyesha umuhimu wa
fani za kiutendi, kubainisha kuwepo au kutokuwepo kwa fani za kiutendi katika
nyimbo za harusi na kuonyesha nyimbo mbalimbali zinazoimbwa katika sherehe za
harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta.Dira iliyotuongoza kuangazia
mada yetu ni nadharia ya Sosholojia ya Utendaji iliyoasisiwa na Bronislaw
Malinowski kutoka Uholanzi na Radcliffe-Brown kutoka Uingereza.Vile vile
tulitumia mtazamo wa viziada lugha wa Okpewho (1992) katika kuelezea fani za
kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na
Wataveta.Katika utafiti wetu tuliongozwa na nadharia tete mbili.Kwanza, tulitaka
kubainisha ya kwamba fani za kiutendi ni za aina mbalimbali katika jamii ya
Wataveta na ile ya Waswahili.Pili, tulitaka kudhibitisha ya kwamba fani za kiutendi
katika nyimbo za harusi zina uhusiano miongoni mwa jamii ya Wataveta na ile ya
Waswahili.Mbinu ya utafiti iliyotumiwa ni ile ya sampuli lengwa.Tuliweza
kutembelea maktabani na kusoma baadhi ya tasnifu zilizoandikwa.Ushauri wa
wahadhiri wetu ulitufaa sana kwani ulikuwa mhimili mkuu wa kazi hii.Utafiti wetu
ulimalizikia nyanjani ambapo tuliwahoji watu kumi wenye umri kati ya miaka
thelathini hadi themanini(30-80) kutoka katika jamii ya Wataveta na ile ya
Waswahili.Tulihudhuria harusi tatu kutoka katika jamii hizi na tukachagua nyimbo
tano (5) kutoka kila jamii.Utafiti huu umedhihirisha kuwepo kwa uhusiano katika fani
za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii hizi mbili kama vile:
minenguo ya mwili,kiitikio,kunyamaza kimya na ishara za uso.Utafiti huu pia
umebaini ya kuwa kuna fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii
hizi mbili ambazo hazina uhusiano, kama vile: maleba na matumizi ya vidole na
mikono | en_US |