dc.description.abstract | Katika utafiti huu tunalenga kuchanganua vibonzo katika gazeti la Taifa Leo. Matumizi ya
mikakati ya vibonzo katika diskosi huweza kuzua utata katika kufasiri ujumbe ulionuiwa
kumfikia msomaji. Tamko la msemaji au mwandishi fulani huweza kufasiriwa na msomaji
kwa njia mbalimbali hasa wanapotumia vibonzo kuwasilisha ujumbe wao. Hali kama hii
huibua hisia mbalimbali kulingana na ujumbe ulioko pale na hata kutatua mawasiliano.
Utafiti huu ulinuiwa kubaini jinsi ambavyo vibonzo vinavyodhihirika katika kuleta dhana ya
Ugatuzi kwenye gazeti la Taifa Leo. Vilevile utafiti huu umenuiwa kuonyesha jinsi mikakati
hiyo inavyoathiri ufasiri wa ujumbe unaodhamiriwa na mwandishi wa vibonzo; malengo ya
utafiti huu ni kuchanganua vibonzo vinavyobeba maudhui ya Ugatuzi, kuchunguza mbinu ya
lugha inayopendelewa sana katika kuwasilishavibonzo hivyo na kuchanganua mitindo ya
lugha inayotumika katika utunzi wa vibonzo hivyo. Nadharia ya Utambulisho/ Ujihusishaji
ya Giles imetuongoza katika utafiti huu. Data kuhusu vibonzo vinavyoleta dhana ya Ugatuzi
vimekusanywa kwa njia ya uchanganuzi wa yaliyomo ambapo nakala 50 za magazeti ya
Taifa Leo ya mwaka 2010-2014 zilihusishwa . Mikakati mbalimbali ya kipragmatiki kama
vile , matumizi ya jazanda, kinaya, chuku, sitiari, yote yaliweza kubainishwa. Aidha utafiti
huu umedhihirisha kuwa matumizi ya kinaya na jazanda katika vibonzo juu ya Ugatuzi ndiyo
iko katika kiwango cha juu zaidi kwa asilimia 64% na mengine kuchukua yaliyosalia. | en_US |