Show simple item record

dc.contributor.authorKilonzo, Peter K
dc.date.accessioned2016-04-21T09:29:14Z
dc.date.available2016-04-21T09:29:14Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/94555
dc.description.abstractDhamira ya utafiti huu ilikuwa ni kuchanganua ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika riwaya ya Maisha Kitendawili ya John Habwe. Mada ilichaguliwa kwa misingi kwamba kazi za kifasihi huibua ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia tofauti. Dira iliyotuongoza kuifanyia utafiti riwaya hii ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Vuguvugu la ufeministi huwa na nadharia nyingi kama vile Ufeministi wa Uingereza, Ufeministi wa Ufaranza, Ufeministi wa Marekani, Ufeministi wa kibidhaa, Ufeministi wa kitamaduni miongoni mwa aina nyingine. Tuliuteua Ufeministi wa Kiafrika kama msingi wa kuifanyia riwaya hii utafiti kutokana na ukweli kuwa imeandikwa kwa misingi ya Kiafrika. Nadharia hii huonyesha jinsi asasi tofauti katika jamii zinavyopelekea kuwako kwa udhalimu wa kijinsia. Pia, nadharia hii hupendekeza mbinu za kupigania ukombozi wa kijinsia katika jamii. Malengo ambayo tuliyaangalia ni jinsi ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia unaathiriwa na asasi za kijamii, jinsi umri tofauti tofauti unavyoathiri ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika jamii inayomkandamiza mwanamke na ujitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika kupigania ukombozi. Mbinu tuliyoitumia katika utafiti huu ni ile ya kukusanya matini za data ya utafiti kutoka vitabuni maktabani. Matokeo ya utafiti wetu ni kuwa, asasi za kijamii kama vile utamaduni, siasa, uchumi, dini na jamii hupelekea kuwako wa udhalimu wa kijinsia. Aidha, tuliona kuwa kuna njia mbalimbali zinazotumiwa ili kuleta ukombozi wa kijinsia.en_US
dc.language.isokiswahilien_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleUjitambuzi na utambulisho wa kijinsia katika riwaya ya maisha kitendawilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record