Show simple item record

dc.contributor.authorKamwanza, Rosemary M
dc.date.accessioned2016-04-21T11:37:55Z
dc.date.available2016-04-21T11:37:55Z
dc.date.issued2015-07
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/94610
dc.description.abstractMadhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza uwasilishwaji wa wahusika wa kike kimajukumu katika Mbali na Nyumbani kwa lengo la kubainisha kuwepo na “kutokuwepo” kwao kwa uwazi katika baadhi ya miktadha na “kutokuwepo” kwao kwa uwazi katika miktadha mingine. Ubainishaji huu ulilenga kuonyesha sababu nzuri na chanya za kihistoria na kianthropolojia ambazo zinaeleza uwasilishwaji wa aina hiyo. Tulidurusu kazi mbali mbali ambazo zimechunguza masuala ya usawiri na taswira ya wanawake ili tufahamu jinsi tathmini zimehitishwa. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni tapo la anthropolojia ambalo ni anthropolojia ya kiutamaduni na kijamii. Nadharia hii inatambua kuchunguzwa kwa masuala ya wanawake kihistoria, uhalisi wa maisha katika jamii na michakato ya kianthropolojia ili kuwapa wanawake tathmini chanya. Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kwamba, sababu za kuwepo na “kutokuwepo” kwa wahusika wa kike katika mazingira na miktadha katika Mbali na Nyumbani ni za kihistoria na kianthropolojia bali sio za kiusawiri. Utafiti ulionyesha pia kwamba, baadhi ya tathmini hasi katika tafiti za awali zinaweza kufikiriwa upya.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleKuwepo ‘kutokuwepo’ kwa wahusika wa kike katika tawasifu ya mbali na nyumbani ya adam shafi (2013)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record