Show simple item record

dc.contributor.authorKimani, Pauline W
dc.date.accessioned2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.available2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/9540
dc.description.abstractUtafiti huu unashughulikia arki za simulizi bunilizi katika Utendi wa Mikidadi na Mayasa. Arki ni sifa za usimulizi wa hadithi bunilizi au halisi. ,Ni vipengele vya kimuundo ambavyo hutumika kwa njia tofauti tofauti kulingana na usimulizi husika. Aidha, ni elementi zinazotumika katika usimulizi wa hadithi ili kufanikisha mawasiliano na uelewa wa hadithi husika. Katika utafiti huu tunatumia nadharia ya naratolojia mwegemeo wa Rimmon-Kenan (2002). Tunataka kuchunguza na kuthibitisha kuwa kuna matumizi ya usimulizi katika ushairi kama ilivyo katika riwaya. Tunaigawanya kazi yetu katika sura sita. Katika sura ya kwanza tunajadili somo la utafiti, madhumuni ya utafiti, maswali ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili tunashughulikia usimulizi, usimulizi wa hadithi, sampuli za wasimulizi, viwango vya usimulizi, uhusika wa msimulizi hadithini, uhusika na mhusika, wakati wa usimulizi, utegemefu wa msimulizi na hadhi ya msimulizi. Katika sura ya tatu nayo tunachunguza mpangilio wa matukio katika hadithi ambao umegawanywa katika mikondo mitatu: mpangilio wa matukio katika mfuatano wa wakati, muda katika usimulizi na idadimarudio ya matukio katika hadithi. Tunahakiki mtazamo katika sura ya nne ambao unachukua sura mbalimbali kama vile sura ya mwanda wakati na mwanda mahali, sura ya saikolojia na sura ya itikadi. Katika sura ya tano tunashughulikia uwasilishaji wa usemi na maw.,zo. Tunatalii usemi halisi na mawazo halisi, usemi halisi hum na mawazo halisi hum, usemi taarifa na mawazo taarifa na usemi taarifa hum na mawazo hum. Sura ya sita ni hitimisho la kazi nzima, matokeo ya utafiti na mapendekezo kuhusu tafiti za baadaye.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleArki za simulizi bunilizi katika utendi wa mikidadi na mayasaen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record