Show simple item record

dc.contributor.authorMjomba, Grace W
dc.date.accessioned2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.available2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/9542
dc.description.abstractUtafiti huu ulishughulikia swala la upole katika nyimbo za harusi kutoka jamii ya Wadawida. Tulitumia mtazamo wa nadharia ya upole ya Brown na Levinston (1978) hasa kipengee cha mikakati ya kuokoa uso. Kadhalika utafiti ulituwezesha kubainisha swala la upole katika nyimbo za harusi za Wadawida. Nyimbo hizi husheheni suala la upole kwa madhumuni ya kuokoa nyuso za maarusi na vile vile aila zinazohusika na sherehe hizi kwajumla. Katika sura ya kwanza tulielezea kwa ufupi kuhusu kiunzi cha mada ya utafiti. Tulielezea tatizo la utafiti na vile vile kuorodhesha madhumuni ya utafiti huu. Pia tuliangazia sababu za kuchagua mada,nadharia tete upeo na mipaka ya utafiti huu, msingi wa nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada na njia za utafiti zilizotuelekeza katika ukusanyaji data. Sura ya pili, tulishughulikia nyimbo tofauti tofauti na majukumu yake kwa ujumla katika jamii ya Afrika. Sura ya tatu na ya nne tulibainisha kuwepo kwa suala la upole katika nyimbo za jamii ya Wadawida baada ya kuzieka katika makundi matatu.katika sura ya tano tumehitimisha na kutoa mapendekezo yatakayowasaidia wasomi wengine.en_US
dc.language.isoothersen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleSuala la upole katika nyimbo za harusi za Wadawidaen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record