Show simple item record

dc.contributor.authorMigiro, Nixon O
dc.date.accessioned2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.available2013-02-12T14:48:06Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/9545
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu motifu za usufi katika Utenzi wa Kiokozi ella Banati, nakala tunayoitumia ni ya Prof. Kineene wa Mutiso, mtunzi wa kazi hiyo ni Sheikh Muhammad Njambeini. Tutatumia nadharia moja ambayo ni Udhanaishi wa kifeministi. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Katika sura ya kwanza tumejadili masuala ya utangulizi wa utafiti. Tumezungumzia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, misingi ya kinadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na njia za utafiti. Katika sura ya pili, tumejadili maana ya usufi, sufi ni nani, chanzo cha usufi, historia fupi ya usufi, mihimili mikuu ya imani ya usufi na usufu katika Afrika Mashariki. Katika sura ya tatu, tumejadili maana ya motifu na motifu za imani ya usufi zilizomo katika Utenzi wa Kiokozi cha Banati. Motifu hizo ni umoja wa Allah, safari ya imani, vitabu, malaika, mitume na nyumba ya Mtume Muhammad. Katika sura ya nne, na tumejadili Nguzo za Uislamu kama motifu za usufi ambazo pia huwa katika Uislamu wa kawaida. Tumesawiri nguzo ya Shahada, Sala, Swaumu, Zaka na Hija. Tumeangazia fadhila na faradhi zao. Motifu hizi huwa na hadhi tofauti kati ya makundi haya mawili, ambayo lengo lao ni kumhudumia Allah. Katika sura ya tano, tumejadili motifu za taratibu na mazoea ya im~ni ya usufi ambayo ,hushughulikia maisha ya waumini katika jamii. Taratibu za janaizi na eda ya kifo na tal aka pamoja na fadhila zao. Sura ya sita, tumetoa hitimisho na tathimini ya madhumuni na nadharia tete na mapendekezo ya utafiti zaidi, kutokana na utafiti huu tumebaini kuwa motifu mbalimbali za usufi zilizomo katika Utenzi wa Kiokozi cha Banati zinatokana na misingi ' ya imani na mwongozo uliomo katika kielelezoasili cha Kurani Takatifu pamoja na Sunna na Hadhithi za Mtume Muhammad (S.A. W).en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleMotifu za usufi katika utenzi wa Kiokozi cha banatien_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record