Show simple item record

dc.contributor.authorGatakaa, Geoffrey
dc.date.accessioned2013-02-12T14:48:07Z
dc.date.available2013-02-12T14:48:07Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/9547
dc.description.abstractKatika utafiti huu tunalenga kuchanganua grafiti ya maktaba za Chuo Kikuu cha Nairobi nehini Kenya tukiongozwa na nadharia ya Utambulisho. Utafiti huu ulihusu grafiti ya maktaba kwenye dawati za kusomea, katika maktaba za Jomo Kenyatta Memorial tl.ibrary (JKML), Chiromo na Umatibabu. Utafiti huu ulikuwa unachunguza haipothesia tatu kwamba; a) Maudhui ya ngono na masomo yanatawala katika grafiti ya maktaba za Chuo Kikuu cha Nairobi, b) Sheng ndiyo lugha inayopendelewa sana katika grafiti ya maktaba za Chuo Kikuu eha Nairobi na c) Mazungumzo, lugha ya kitamathali na ukiushindiyo mitindo ambayo inatumika sana katika grafiti ya maktaba za Chuo Kikuu cha Nairobi. Data ilikusanywa kutoka kwenye madawati ya maktaba tatu za Chuo Kikuu cha Nairobi. Kutokana na data hii, sampuli yajumbe 100 ilichaguliwa iii kuchanganuliwa. Data ilichanganuliwa kwa kutumia majedwali na vielelezo vya nambari na maelezo ya matokeo kujadiliwa. Utafiti huu umegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti na katika sura ya pili tumejadili kwa kina suala zima la grafiti. Katika sura ya tatu tumeainisha maudhui na sura ya IIDe tukaainisha lugha zilizotumika katika grafiti ya maktaba. Tumechunguza mitindo ya lugha katika sura ya tano. Mwishowe tukatoa muhtasari, hitimisho, ehangamoto za utafiti na mapendekezo katika sura ya sita. Matokeo ya uchanganuzi yameonyesha kuwa maudhui ya ngono na masomo yametawala katika grafiti ya maktaba; hivyo kuunga mkono haipothesia yetu ya kwanza. Pia, matokeo yameonyesha kuwa lugha ya Kiingereza ndiyo lugha ambayo inapendelewa sana katika uandishi wa grafiti ya maktaba, matokeo ambayo yanapinga haipothesia ya pili. Zaidi ya haya, tumegundua kuwa mitindo ya mazungumzo, ukiushi na matumizi ya tamathali za lugha ndiyo imetumika sana, kumaanisha kuwa haipothesia ya tatll ni ya ukweli.en_US
dc.language.isoen_USen_US
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen_US
dc.titleUhakiki wa maudhui teule katika utendi wa mikidadi na mayasaen_US
dc.title.alternativeThesis (MA)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record