Abstract
Makala haya yanaeleza umuhimu wa vazi la kanga au leso kama njia ya kupitisha jumbe za aina aina katika maisha ya Msawhili.Tumeeleza umbo la kanga,matumizi yake anuwai na maneno ('majina') yake tofauti tofaiti ambayo huwa aidha ya kishauri au kinathari.Maneno na kauli hizo hurejelea jumbe za kidini,harusi,maneno ya kawaida ya hekima,tahadhari na kuonya,kupongeza,wazazi na mapenzi yao yasopimika na moyo wao wa kujali,kati ya maudhui mengine.