Show simple item record

dc.contributor.authorMunga, Duncan S
dc.date.accessioned2016-11-14T11:05:05Z
dc.date.available2016-11-14T11:05:05Z
dc.date.issued2015-11
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97095
dc.description.abstractWarabai ni mojawapo wa makabila yanayoungana pamoja kuunda kundi moja lijulikanalo kama Mijikenda. Baadhi ya makabila yanayounda kundi la Mijikenda ni pamoja na Waribe, Wagiriama ambao ni wengi kuliko makabila mengine ambayo ni pamoja na Wakauma, Wajibana, Wachonyi, Wakambe na Warabai wanaopatikana katika kaunti ya Kilifi na kunayo makundi yanayopatikana katika kaunti ya Kwale. Nao ni Wadigo na Waduruma. Wote wakiwa makabila tisa wakiitwa Wamijikenda, ni Wabantu ambao chimbuko lao ni msitu wa Kongo ulioko Afrika ya Kati. Walitoka Kongo kwa sababu ya kutafuta makaazi mapya baada ya idadi ya wabantu walioishi huko kuongezeka. Kila kundi la wabantu walipotoka Kongo walishika njia yao. Hii ilipelekea kufika sehemu wanamoishi sasa. Hapa walikuja kuwa na ujirani na Waswahili ambao ni wabantu pia. Waswahili kama vile Wamijikenda wana makabila kumi na mawili. Makabila haya kumi na mawili ya Waswahili ndiyo yaliyokuwa na idadi kubwa ya wakaazi wa kisiwa cha Mombasa. Kulikuwa namuunganowa makabila matatu ya Wakilindini, Wachangamwe, Watangana (miji mitatu). Makabila ya Mvita yaliundwa na Wamvita, Wakilifi, Wamtwapa, Wapate, Washaka, Wagunya, Wakatwa, Wafaza, na Wajomvu. Majina ya makabila haya yatujulisha kwamba takribani saba yao, tukitenga Wa-mvita na Wajomvu yalitoka makao ya zamani ya Waswahili kaskazini mwa Mombasa. Wajomvu wanao julikana kwa ujuzi wao wa kutengeneza vyungu Pwani. Bado wanaishi katika makaazi yao yapatikanayo kando kando ya mkondo wa Bahari Hindi Mombasa ui twao Maungunja na Jomvu Kuu. vi Wanaongea lafudhi iliyo tofauti na ya Kiswahili cha Ki-mvita. Na yale makabila matatu yaliundwa na Wa-kilindini, Wa-changamwe na Wa-tangana. Kando na makabila kumi na mawili ya Waswahili walikuwa na urafiki na Wamijikenda wa Nyika.Wamijikenda walichangia sana katika siasa na vita vya Mombasa. Kwa vile walikuwa wajuzi wa kutumia upinde na mishale walikuwa jeshi muhimu la Mombasa katika vita na Wapate na Waomani. Hii ilikuwa sababu mojawapo ya ushirikiano baina yaWaswahili na Wamijikenda, pamoja na kuoleana mabinti zao. Hii ilisababisha Wanyika (Wamijikenda) kuwaita Waswahili ‟adzomba‟ kumaanisha wajomba na wapwa. Wamijikenda waliuzia watu wa Mombasa bidhaa nyingi kama vile „gumcopal‟. Ushirikiano baina ya Waswahili na Wamijikenda ulifanikishwa na wazee wamiji kama vile Tamimu aliyekuwa mmoja wa yale makabila matatu ya Waswahili. Kwa hivyo tunaona makundi haya mawili ya Wamijikenda na Waswahili waliokuwa na ushirikiano mwafaka ndio sababu tukatafiti juu ya miiko na tasfida yao na tukalinganisha Tulijikita katika Warabai kwa niaba ya Wamijikenda na Wajomvu kwa niaba ya Waswahili kwani hawa wameishi kwa ujirani wa tokea kale. Utafiti huu unahusu uwasilishaji na majukumu ya Miiko na Tasfida ya Warabai na Waswahili. Kazi hii imegawanyika katika sura nne. Katika sura ya kwanza tumeangazia maswala muhimu ya utafiti wetu. Tumeelezea swala la utafiti, madhumuni na nadharia tete zilizotuongoza. Aidha, sababu za utafiti na upeo na mipaka zimeelezwa. Msingi wa nadharia wa utafiti umefafanuliwa, na yaliyoandikwa kuhusu mada yalijadiliwa. vii Mwisho, mbinu za utafiti zimebainishwa na uwasilishaji wa data umefanywa. Katika sura ya pili, tumeshughulikia fasili na asili ya Miiko na Tasfida ya Warabai na Waswahili. Aidha, katika sura ya tatu, tumezungumzia misamiati ya Miiko naTasfida ya Warabaina vilevile Waswahili. Pia tumeshughulikia mikakati ya matumizi ya Miiko na Tasfida. Pia tumeshughulikia majukumu yanayojitokeza katika Miiko naTasfida ya Warabai na Waswahili.Sura ya nne, ambayo ndio mwisho, tumejikita katika matokeo ya utafiti, changamoto tulizokumbana nazo. Pia tumetoa mapendekezo ya utafiti wa baadaye kuhusu mada hii.Msingi wa nadharia uliotumiwa ni wa nadharia ya upole ya Brown na Levinson (1987). Lengo la utafiti huu ni kuchunguza na kufafanua miiko na tasfida itumiwayo sana na Warabai na vile vile Waswahili, ili kuasisi taarifa na maana za tasfida na miiko ya lugha ya Kirabai na Waswahili, kuchunguza majukumu ya Miiko na Tasfida zitumiwazo na Warabai na Waswahili. Data ya utafiti ilikusanywa kutoka kwa watafitiwa ishirini wake kwa waume Warabai wa kutoka kata ndogo ya Rabai, wilaya ya Rabai na Gatuzi la Kilifi na vilevile Waswahili wa Jomvu Gatuzi la Mombasa. Hii ni kwa sababu kwamba mtafiti ni mzungumzaji wa lugha ya Kirabai izungumzwayo Gatuzi la Kilifi. Pia kuhoji watafitiwa Wajomvu. Matokeo yaonyesha kwamba ili kuepuka kufedhehesha, Warabai na Waswahili hujaribu kutafuta maneno mbadala ambayo huficha aibu kuliko kutumia maneno ya miiko. Hivyo basi hutumia tasfida kuepuka yale maneno ya aibu na yawezayo kuleta aibu kwa mzungumzaji wa Kirabai.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.subjectMiiko na tasfidaen_US
dc.titleKulinganisha Miiko Na Tasfida Ya Waswahili (Wajomvu) Na Warabaien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record