Show simple item record

dc.contributor.authorMwangi, Waweru D
dc.date.accessioned2016-11-15T05:48:44Z
dc.date.available2016-11-15T05:48:44Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97178
dc.description.abstractKatika utafiti wetu tumeangazia changamoto na manufaa ya kutafsiri Kiswahili katika miktadha ya wingilugha. Tulichagua hii mada ili kuweka wazi changamoto zinazokumba shughuli za kutafsiri . Vile vile tulitaka kubainisha manufaa yanayotokana na kutafsiri Kiswahili katika miktadha ya wingilugha. Ili kufikia malengo yetu tuliongozwa na nadharia ya mawasiliano katika tafsiri iliyoasisiwa na Peter Newmark (1982). Nadharia hii ilitufaa kwa sababu, kwa ujumla inaangazia suala la kuimarisha na kufanikisha mawasiliano katika mchakato wa kutafsiri. Baadhi ya changamoto ambazo tuliweza kugundua katika utafiti wetu ni changamoto zinazosababishwa na mifanyiko ya kitamaduni. Tumetoa mifano ya baadhi ya tamaduni hizi kwa mfano; aina ya vyakula, aina ya mavazi na mapambo, majina ya kurejelea wapendwa katika jamii, kuzawadiana katika jamii na kadhalika. Tumetoa mifano katika lugha ya Kimaasai na kulinganisha na lugha ya Kiswahili.Tuliteua lugha ya Kimaasai kwa sababu ndio lugha inayotumika na wengi na pia ndio lugha ya wenyeji wa maeneo yetu ya utafiti ya wilaya ya Narok Kaskazini. Pia katika kuangazia changamoto katika kutafsiri, tuligundua changamoto zinazosababishwa na tofauti za miundo ya lugha na tumetoa mifano maridhawa. Pia katika utafiti wetu, tumegundua licha ya kuwa kuna changamoto ya kutafsiri kuna manufaa pia. Tumeangazia manufaa hayo kwa kutoa mifano mwafaka. Tuliteuwa sekta muhimu katika maeneo yetu ya utafiti ambazo ni sekta za elimu, dini na sekta ya afya au matibabu.Tuligundua kwamba tafsiri inachangia pakubwa katika kuimarisha mawasiliano katika sekta hizi muhimu.Tumetamatisha kazi yetu kwa kutoa mapendekezo manne. Kwanza, tulipendekeza manufaa ya kutafsiri yachunguzwe katika sekta ya biashara kwa sababu sekta hii ni muhimu sana na inahusisha watu wengi katika jamii yoyote ile. Pili, tulipendekeza kwamba, kwa sababu tumejikita katika maeneo ya Narok Kaskaszini, maeneo mengine yatafitiwe. Pia tumependekeza tafiti zaidi zifanywe kuhusu tafsiri ili kupendekeza na kuthibitisha umuhimu wa kuanzisha somo la tafsiri katika shule za msingi na za upili na suala hili lichukuliwe kuwa suala nyeti. Hatimaye tumependekeza kando na nadharia ya mawasiliano katika tafsiri, nadharia zingine zitumiwe katika tafiti zingine za tafsiri ili kubainisha manufaa na changamoto katika mchakato wa kutafsiri.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleChangamoto Na Manufaa Ya Kutafsiri Kiswahili Katika Miktadha Ya Wingilugha Narok Kaskazinien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States