Show simple item record

dc.contributor.authorGwako, Jackline B
dc.date.accessioned2016-11-15T08:46:02Z
dc.date.available2016-11-15T08:46:02Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97251
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia maadili kwa vijana wa kiume yanayojitokeza katika tenzi za Siraji na Adili. Katika utafiti huu tumeongozwa na nadharia ya maadili ambayo inalenga kazi za fasihi kutatua matatizo ya jamii kwa njia ipasavyo na kujenga jamii bora yenye maelewano. Malengo ya utafiti wetu ni kuangalia jinsi ambavyo watunzi Kijumwa na Robert wa utenzi Siraji na Adili wamelishughulikia swala la maadili kwa vijana wa kiume katika tenzi hizo. Aidha, tumelinganisha na kulinganua jinsi watunzi Kijumwa na Robert wamelishughulikia swala la maadili kwa vijana wa kiume katika tenzi hizo na hatimaye tumebaini sababu za kuwiana na kutofautiana kwao. Baada ya kufanya utafiti wetu kwa kusoma na kuzichambua tenzi- Siraji na Adili tumebaini ya kwamba makisio yetu kuwa watunzi Kijumwa na Robert wameyashughulikia maadili kwa vijana wa kiume ni ukweli na pia wamewiana na kutofautiana kwa njia moja au nyingine. Hatimaye tumeweza kubaini ya kwamba ni ukweli tenzi hizi zina uhusiano wa karibu sana kwa sababu watunzi Kijumwa na Robert wameyafungamanisha maadili hayo na mafunzo ya dini ya Kiislamu ndiposa tukachanganua data yetu kwa njia ya maelezo na ufafanuzi huku tukitoa thibitisho kutoka kwa tenzi- Siraji na Adili pamoja na Kurani Takatifu. Aidha, tumepata kuwa kutofautiana kwa watunzi kunatokana na maoni yao ya kibinafsi, na tajriba walionazo kutegemea mazingira waliokulia.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisheruniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectMaadili Kwa Vijana Wa Kiume Katika Tenzi Mbilien_US
dc.titleUchanganuzi Linganishi Wa Swala La Maadili Kwa Vijana Wa Kiume Katika Tenzi Mbili: Siraji Na Adilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States