Show simple item record

dc.contributor.authorNyagah, Shadrack Kirimi
dc.date.accessioned2016-11-23T07:10:13Z
dc.date.available2016-11-23T07:10:13Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/97743
dc.description.abstractUtafiti huu unalenga kuchanganua na kubainisha makosa ya kifonolojia na kimofolojia yanayojitokeza katika kazi andishi za wanafunzi wa shule za upili za Tigania jimboni Meru. Ili kufanikisha lengo hili, data ilikusanywa kutoka shule mbili za mseto na kuchanganuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya Lugha-Kati ya Selinker (1972). Uchunguzi huu ulinuia kujaribisha nadharia tete zifuatazo: a) Kazi zilizoandikwa na wanafunzi wa kidato cha pili huwa na makosa mbalimbali ya kifonolojia na kimofolojia. b) Uhawilishaji wa lugha ya kwanza hadi lugha ya pili ndicho kiini kikuu cha makosa ya kifonolojia na kimofolojia. c) Makosa mengi hujitokeza katika kategoria ya vitenzi kuliko kategoria nyingine na d) Zaidi ya asilimia 50% ya makosa itadhihirika katika kazi za wanafunzi wa kiume ikilinganishwa na wenzao wa kike. Matokeo ya uchunguzi huu yalidhihirisha kwamba aina mbalimbali za makosa hujitokeza kwenye insha za wanafunzi. Baadhi ya makosa haya ni pamoja na yale ya unazalishaji wa fonimu, udondoshaji wa sauti, uchopekaji wa irabu na utumiaji wa sauti mbadala. Pia kuna makosa yaliyotokana na uambishaji na unyambuaji pamoja na mlandano wa kiumbo. Chanzo kikuu cha makosa haya kilibainishwa kuwa athari ya lugha ya kwanza kwa kujizolea frikwezi ya asilia 60%. Vyanzo vingine yaani: ujumlishaji mno, mikakati ya mawasiliano, mikakati ya kujifunza L2 na uhawilishaji wa ufundishwaji viliandikisha asilimia 40% iliyosalia. Aidha, kategoria ya vitenzi iliandikisha frikwenzi ya juu zaidi ya 309 kwa 613 ya jumla ya makosa ambayo ni sawa na asilimia 50.41%. Vilevile, jinsia ya kiume iliandikisha asilimia 53.67% ya makosa nayo ile ya kike ikaandikisha asilimia 46.33%. Isitoshe, mikakati na mbinu anuai zinazoweza kutumiwa kukabili makosa haya zimependekezwa.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleUchanganuzi Wa Makosa Ya Kifonolojia Na Kimofolojia Yanayojitokeza Katika Kazi Andishi Za Wanafunzi Wa Shule Za Upili, Tigania, Jimbo La Meruen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record