Show simple item record

dc.contributor.authorMekonge, L. N
dc.date.accessioned2016-12-22T11:22:27Z
dc.date.available2016-12-22T11:22:27Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/98308
dc.description.abstractUtafiti huu ulihusu athari za Sheng katika ufundishaji wa Kiswahili katika shule za upili za Gusii Highlights na Daraja mbili mjini Kisii. Kuwepo kwa matokeo yasiyoridhisha katika somo la Kiswahili katika miaka ya hivi karibuni katika shule hizi kulihitaji utafiti ili kubaini sababu za kutokea kwa hali hii. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchanganua makosa ya kimofolojia na kisemantiki yanayojitokeza katika kazi za Kiswahili zilizoandikwa na wanafunzi wa shule hizi. Utafiti huu ulitathmini ni kwa kiwango gani Sheng huchangia kutokea kwa makosa hayo. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, baadhi ya wanafunzi kutoka vidato vyote vinne vya usomi katika shule hizi waliandika insha zilizosahihishwa na makosa yaliyopatikana yanayotokana na Sheng yalichanganuliwa kwa misingi ya mtazamo wa Uchanganuzi Makosa na Lugha Kadirifu. Makosa hayo yaliainishwa katika kategoria mbalimbali kisha visababishi vya makosa hayo viliweza kubainishwa. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwepo kwa makosa hayo katika vidato vyote japo kwa asilimia tofauti tofauti. Matokeo haya yalibaini kuwa kadri mwanafunzi anavyoendelea na masomo katika vidato vya juu, makosa yanayotokana na Sheng huongezeka. Sheng imechangia pakubwa kutokea kwa makosa haya. Pia utafiti huu ulibaini mikakati ya kuzuia kutokea kwa makosa haya.en_US
dc.language.isoOthersen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectAthari Za Sheng Katika Ufundishaji Wa Kiswahili Mjini Kisii: Utafiti Kifani Wa Shule Za Upili Za Gusii Highlights Na Daraja Mbili.en_US
dc.titleAthari Za Sheng Katika Ufundishaji Wa Kiswahili Mjini Kisii: Utafiti Kifani Wa Shule Za Upili Za Gusii Highlights Na Daraja Mbili.en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States