Show simple item record

dc.contributor.authorBosibori, Bosire T
dc.date.accessioned2016-12-23T09:36:57Z
dc.date.available2016-12-23T09:36:57Z
dc.date.issued2016
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/98507
dc.description.abstractTamthilia ya Kiswahili ni mojawapo ya tanzu za Fasihi Andishi ya Kiswahili. Tanzu nyingine ni pamoja na riwaya, ushairi, hadithi fupi, novela na zinginezo. Utanzu wa tamthilia umedhihirisha kwa njia moja au nyingine uhusiano wa kimwingilianomatini. Utafiti huu umelenga kuchunguza na kuchanganua mwingilianomatini kati ya tamthilia za Mstahiki Meya (Arege,2009) na Mkaguzi Mkuu wa serikali (Gogol,1979). Katika kuhakiki hayo, tumetumia nadharia ya Mwingilianomatini iliyoasisiwa na mwana nadharia wa Kifaransa Julia Kristeva. Tumeongozwa na malengo matatu ya utafiti-kuchunguza jinsi tamthilia zinavyoingiliana kifani na kimaudhui vilevile kuchunguza iwapo nadharia ya Mwingilianomatini inafaa katika uhakiki wa tamthilia ya Kiswahili. Utafiti umeongozwa na maswali yafuatayo: Je, tamthilia hizi zina mwingiliano au la, zikiwa zinao, basi kwa kiwango gani? Je, ni sehemu zipi za tamthilia zinaingiliana kwa mujibu wa mwanda wa mwingilianomatini? Kutokana na utafiti huu, imebainika wazi kwamba tamthilia ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali na Mstahiki Meya zinaingiliana katika vipengele vya msuko, usawiri wa wahusika, mandhari na maudhui. Maswali yetu ya utafiti yamepata kujibiwa kikamilifu kwa kuwa tumeweza kuonyesha jinsi tamthilia zinavyoingiliana na kuchangizana. Hatimaye, tumetoa mapendekezo kwa watakaofanya tafiti za baadaye kuhusiana na swala la kuingiliana kwa matinien_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectMwingilianomatini Kati Ya Mkaguzi Mkuu Wa Serikali Na Mstahiki Meyaen_US
dc.titleMwingilianomatini Kati Ya Mkaguzi Mkuu Wa Serikali Na Mstahiki Meyaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States