Usawiri wa Mtume Muhammadi Katika Ukawafi wa Miiraji na Mafunzo Yake kwa Wafuasi Wake.
View/ Open
Date
2016Author
Wathe, Silveria N
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchanganua usawiri wa Mtume Muhammadi (S. A. W) katika Ukawafi wa Miiraji na Mafunzo yake kwa wafuasi wake. Mada hii ilichaguliwa kwa misingi kwamba Mtume Muhammadi ni jagina katika dini ya Kiislamu. Mtume huyu alienda safari ya ajabu usiku mmoja katika ulimwengu mwingine, na akawaletea wafuasi wake zawadi ya sala tano. Utafiti huu ulilenga kubainisha kuwa mtunzi wa ukawafi wa miiraji amemsawiri Mtume Muhammadi (S. A. W) kama jagina wa kidini. Nadharia ya uamilifu ilitumika kwa sababu ilionekana kufaa zaidi kuchanganua usawiri wa Mtume Muhammadi (S. A. W) katika ukawafi wa miiraji na mafunzo yake kwa wafuasi wake, kwani ujagina ni mojawapo wa asasi ambazo huzuka katika jamii ili kuyatatua matatizo yanayoikumba jamii husika. Shida ambazo jamii hupitia huwa haziondoki hadi pale ambapo jagina ataibuka na kuziondoa. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchanganua usawiri wa Mtume Muhammadi (S. A. W) katika utenzi ulioteuliwa na kueleza mafunzo yake kwa wafuasi wake. Matokeo ya utafiti huu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima wa utafiti huu. Utafiti wetu umebainisha kwamba usawiri wa Mtume Muhammadi (S. A. W) katika utenzi huu unadhihirisha kwamba, yeye ni jagina katika dini ya Kiislamu. Aidha, tumebainisha kwamba safari ya Mtume Muhammadi (S. A. W) ina mafunzo mengi kwa wafuasi wake kama vile, miji mitakatifu, mitume katika dini ya Kiislamu, tofauti kati ya dini ya Kiislamu na dini zingine na uwezo wake Mwenyezi Mungu.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Usawiri Wa Mtume MuhammadiRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: