Uchanganuzi Linganishi Wa Swala La Maadili Kwa Vijana Wa Kiume Katika Tenzi Mbili: Siraji Na Adili

View/ Open
Date
2016Author
Gwako, Jackline B.
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia maadili kwa vijana wa kiume yanayojitokeza katika tenzi za
Siraji na Adili. Katika utafiti huu tumeongozwa na nadharia ya maadili ambayo inalenga
kazi za fasihi kutatua matatizo ya jamii kwa njia ipasavyo na kujenga jamii bora yenye
maelewano. Malengo ya utafiti wetu ni kuangalia jinsi ambavyo watunzi Kijumwa na
Robert wa utenzi Siraji na Adili wamelishughulikia swala la maadili kwa vijana wa
kiume katika tenzi hizo. Aidha, tumelinganisha na kulinganua jinsi watunzi Kijumwa na
Robert wamelishughulikia swala la maadili kwa vijana wa kiume katika tenzi hizo na
hatimaye tumebaini sababu za kuwiana na kutofautiana kwao. Baada ya kufanya utafiti
wetu kwa kusoma na kuzichambua tenzi- Siraji na Adili tumebaini ya kwamba makisio
yetu kuwa watunzi Kijumwa na Robert wameyashughulikia maadili kwa vijana wa kiume
ni ukweli na pia wamewiana na kutofautiana kwa njia moja au nyingine. Hatimaye
tumeweza kubaini ya kwamba ni ukweli tenzi hizi zina uhusiano wa karibu sana kwa
sababu watunzi Kijumwa na Robert wameyafungamanisha maadili hayo na mafunzo ya
dini ya Kiislamu ndiposa tukachanganua data yetu kwa njia ya maelezo na ufafanuzi
huku tukitoa thibitisho kutoka kwa tenzi- Siraji na Adili pamoja na Kurani Takatifu.
Aidha, tumepata kuwa kutofautiana kwa watunzi kunatokana na maoni yao ya kibinafsi,
na tajriba walionazo kutegemea mazingira waliokulia.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Uchanganuzi Linganishi Wa Swala La Maadili Kwa Vijana Wa Kiume Katika Tenzi Mbili: Siraji Na AdiliRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: