Nafasi Ya Vijana Katika Riwaya Za Pendo La Karaha Na Kovu Moyoni
Abstract
Tumeangazia nafasi ya vijana katika riwaya za Pendo la Karaha na Kovu Moyoni za
John Habwe. Hata hivyo ilitubidi kusoma riwaya nyinginezo za mwandishi huyu
kama vile Hadaa ya Nafsi na Safari ya Lamu ili tupate ufahamu zaidi kuhusu
mwelekeo wa uandishi na falsafa ya msanii huyu. Tulichagua mada ya nafasi ya
vijana katika riwaya zilizohusika, kwanza kwa sababu nafasi ya vijana inaonekana
kudhihirisha na kuakisi hali ilivyo katika jamii zetu. Hii ni kwa sababu jamii zetu zina
mchango mkubwa katika hali ya maisha ya vijana. Tulilenga vilevile kuchunguza
changamoto zinazowakabili vijana katika jamii na kuwazuia katika juhudi zao za
kujikomboa kutoka katika matatizo mengi kama ukosefu wa ajira na usambazaji wa
dawa za kulevya. Aidha ubinafsi, dhuluma za mapenzi kutoka kwa waajiri, unafiki wa
viongozi, utabaka uliokithiri na umaskini ni baadhi tu ya changamoto
wanazokumbana nazo vijana kwenye jamii. Utafiti wetu umeongozwa na nadharia ya
Uhalisia Hakiki tukijikita katika kiunzi chake cha tatu kinachodai kuwa matukio au
mambo yanayotendeka katika jamii hutendeka kwa kusababishwa na mambo fulani
wala hayatokei tu vivi hivi. Kila tukio lina chanzo chake. Mwongozo huo umetufanya
kuitathmini jamii mwanzo kabla ya kuitalii nafasi ya vijana katika riwaya
zinazohusika. Kutokana na utafiti wetu, imebainika kuwa John Habwe amefaulu
vilivyo katika kuwasawiri vijana na nafasi hasi na chanya wanazochukua katika jamii
iliyojaa adha ya ubinafsi, uchochole, udhalimu, utabaka, na unafiki katika kutaja
maovu machache. Aidha mwandishi ametoa mchango wake muhimu katika
kuwajenga vijana kihadhi
Publisher
University of Nairobi
Subject
Riwaya Za PendoRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: